Nenda kwa yaliyomo

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1864

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1864 ulikuwa wa 20 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 8 Novemba. Upande wa "Republican Party" (chini ya jina la "National Union"), Rais Abraham Lincoln (pamoja na kaimu wake Andrew Johnson) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" George McClellan (pamoja na kaimu wake George Pendleton).

Lincoln akapata kura 212, na McClellan 21. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo. Hakuwa na kupiga kura katika majimbo kuminamoja yaliyoasi na Maungano wakati wa vita.