Uchaguzi Mkuu wa Malawi, 2004
Malawi |
Makala hii imepangwa kwa mfululizo: |
|
Nchi zingine · Atlasi |
Uchaguzi wa Urais na Bunge ukifanyika nchini Malawi mnamo 20 Mei 2004. Uchaguzi huu ulikuwa umepangiwa kutendeka mnamo 18 Mei lakini ukahairishwa kwa siku mbili kufuatia mwitikio kwa madai ya wapinzani kuhusu udanganyifu katika sajala ya wapiga kura.[1].
Kufikia 22 Mei, hakuna matokeo yalikuwa yametangazwa, jambo lililoonekana kutishia amani. Mnamo 25 Mei, Tume ya Uchaguzi ya Malawi hatimaye ilitangaza matokeo. Bingu wa Mutharika, mgombezi wa urais kwa chama cha United Democratic Front, alitangazwa kuchaguliwa. Mutharika alikuwa akiungwamkono na rais anayeondoka Bakili Muluzi, ambaye alisaafu baada ya kuhudumu kwa vipindi viwili. Malawi haina Kura za maoni za kutegemewa lakini utafiti uliofanywa na vyombo vyya habari vya Malawi kabla ya uchaguzi ulikuwa umemweka Gwanda Chakuamba, mgombea wa mrengo wa vyama saba kuwa aliyepigiwa upato kuongoza.
Jedwali la Matokeo
[hariri | hariri chanzo]Mgombea | Chama | Kura | % |
---|---|---|---|
Bingu wa Mutharika | United Democratic Front | 1,119,738 | 35.9 |
John Tembo | Malawi Congress Party | 846,457 | 27.1 |
Gwanda Chakuamba | Mgwirizano Coalition | 802,386 | 25.7 |
Brown Mpinganjira | National Democratic Alliance | 272,172 | 8.7 |
Justin Malewezi | People's Progressive Movement | 78,892 | 2.5 |
Invalid/blank votes | 86,218 | - | |
Jumla | 3,205,863 | 100 | |
Chanzo: EISA |
Wagombea Urais
[hariri | hariri chanzo]- Bingu wa Mutharika, mkongwe wa miaka sabini na mwanauchumi, alikuwa mgombea kwa tiketi ya CHama cha United Democratic Front, ingawa awali alikuwa mpinzani wa chama hicho. Aliungwa mkono na rais anayeondoka, Muluzi.
- Gwanda Chakuamba, mwenye umri wa miaka 69, alikuwa akigombea kwa tiketi ya Muungano wa Mgwirizano au Muungano wa Umoja ambao ulishirikisha vyama saba. Chamwamba aliwahi kuwa waziri wa ngazi ya juu na komanda wa jeshi la militia. Mnamo 1980 alizozana na Banda, na akashtakiwa kupanga mauaji yake. Alikaa miaka 12 gerezani na hili likamfanya shujaa maarufu na hatimaye akamrithi Mpanda katika nafasi yake ya uongozi wa Chama chake cha Malawi Congress Party.
- Brown Mpinganjira, wa Umri wa miaka 55, alikuwa mgombea kwa tiketi ya Chama cha National Democratic Alliance, ambacho ni tabaka lililojitoa kwa chama tawala.
- Justin Malewezi, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Malawi chini ya Bakili Muluzi, aligombea urais kutoka chama cha People's Progressive Movement, akiwa amerukwa kugombea kutoka katika chama tawala.
- John Tembo, wa umri wa miaka 72, alikuwa mgombea kutoka chama cha Malawi Congress.
Uchaguzi wa Bunge
[hariri | hariri chanzo]Bunge la Malawi lina wabunge 192. Kulingana na BBC, Chama cha Malawi Congress kilishinda viti ‘’’60’’’, United Democratic Front kikashinda 49, Muungano wa Mgwirizano ukazoa viti 28 na wagombea wa kibinafsi wakanyakua viti 38. Katika Uchaguzi Mkuu wa Malawi wa 1999, United Democratic Front ilikuwa imeshinda viti 93, Malawi Congress Party kikashinda viti 66, huku Alliance for Democracykikishinda viti 29.
Wakaguzi wa Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Tasisi ya Uchaguzi ya Afrika Kusini ilituma wakaguzi nchini Malawi kwa uchaguzi wa urais na bunge wa 2004[2].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Special report on general elections", IRIN, 19 Mei 2004.
- ↑ Ott, Martin. The power of the vote: Malawi's 2004 parliamentary and presidential elections. Kachere Series, 2005. uk. 296. ISBN 9789990876581. Found at Google Books
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Poll favours Chakuamba, Mgwirizano to win Archived 7 Desemba 2004 at the Wayback Machine.
- Mgwirizano Lacks Transparency