UN Women

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

UN Women ni shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika kuwawezesha na kutetea haki na usawa kwa wanawake na wasichana, pamoja na upingaji wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Shirika hili la kimataifa la uwewezeshaji Wanawake Duniani lilianzishwa mnamo mwaka 1976 na kutambuliwa rasmi mwaka 1976 na kuanza kufanya kazi zake rasmi mnamo mwezi Januari mwaka 2011 .[1] Raisi mstaafu wa Chile Michelle Bachelet alikuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika hili, na Sima Sami Bahous ni mkurugenzi mtendaji wa shirika hili kwa sasa.[2] Shirika hili pia ni mwanachama wa kundi la kimaendeleo la umoja wa Mataifa .[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Frequently Asked Questions. UN Women - Asia and the Pacific.
  2. Gender equality ‘champion’ Sima Sami Bahous to lead UN Women (en) (2021-09-13).
  3. UNDG Members. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-05-11. Iliwekwa mnamo 2023-01-16.