Nenda kwa yaliyomo

UKUTA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

UKUTA (kirefu chake: Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania) ni chama kilichoasisiwa na hayati Mathias Mnyampala mnamo mwaka wa 1965. Lengo kuu la kuanzishwa kwa UKUTA lilikuwa kuendeleza ushairi na matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla.[1]

Chama kilinuia kusimamia madhumuni kama vile:

  1. Kuhamasisha matumizi ya Kiswahili fasaha katika jamii
  2. Kutoa miongozo ya utungaji bora wa kazi za fasihi kwa watunzi chipukizi
  3. Kuandaa vitabu vya mashairi ya Kiswahili
  4. Kushirikiana na taasisi nyingine za ukuzaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika kuendeleza lugha ya Kiswahili. Mathalani kupitia semina na makongamano mbalimbali yanayochochea utumizi mkubwa wa Kiswahili.

UKUTA ilikumbwa na changamoto mbalimbali kama zinavyokumbwa taasisi nyingine za Kiswahili katika kutimiza majukumu yake ya kukuza na kueneza matumizi ya lugha ya Kiswahili. Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kwa ajili ya kutatua matatizo yanayohitaji pesa kuyatatua. Ilikuwa lazima ipatikane fedha ili kuweza kutoa machapisho mbalimbali kwa ajili ya semina na makongamano, upungufu wa watalaamu wa fani ya ushairi na kadhalika. Nyengine ilikuwa kupungua kwa utanzu wa ushauri tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Katika kuhakikisha wanafikia malengo, UKUTA iliweza kufanikiwa kuchapisha baadhi ya mashairi kama vile:

  1. Mwaka wa 1977 waliweza kuandika mashairi ya kusifu miaka kumi ya Azimio la Arusha yaliyoitwa Mashairi ya Miaka Kumi ya Azimio la Arusha (UKUTA, 1977) na Ngonjera za UKUTA (1968) kikiwa kama kitabu chao cha kwanza.
  2. Kuandaa na kuendesha makongamano kwa waandishi wachanga ili kuwaelimisha kuhusu mbinu za wa mashairi na ngonjera.
  1. "UKUTA | Swahili poets' association", Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2018-09-02
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu UKUTA kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.