UDA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
UDA
Jina kamiliUnited Democratic Alliance
Jina la utaniWheelbarrow
ImeanzishwaMachi 10, 2021; miaka 2 iliyopita (2021-03-10)
MmilikiWilliam Ruto
MwenyekitiJohnson Muthama

United Democratic Alliance au UDA[1] ni Chama cha kisiasa kinachoongozwa na naibu rais wa kwanza wa taifa la Kenya, William Ruto[2].

Chama hicho kilianzishwa mwaka 2012 kwa jina la Party of Action (POA) kikashiriki uchaguzi wa 2013 kwa kushirikiana na Kenya National Congress (KNC) bila kufaulu, kikabaki bila mbunge.

Chama kilibadilisha jina lake mwaka 2017 na kugombea kwa jina la Party of Development and Reforms (PDR). Katika uchaguzi wa rais kilisimama pamoja na mshindi Uhuru Kenyatta ilhali kikafaulu kupata wabunge wanne na seneta mmoja.

Kwenye mwaka 2020 chama kiliamua kushirikiana na William Ruto kikibadilisha jina lake tena kuwa UDA[3].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. United Democratic Alliance – kazi ni kazi (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-07-01. Iliwekwa mnamo 2022-07-12.
  2. Tokeo la Picha kutoka Google kwa https://uda.ke/site/wp-content/uploads/2021/04/upload.jpg. www.google.com. Iliwekwa mnamo 2022-07-12.
  3. https://www.the-star.co.ke/news/2021-01-25-hustlers-march-inside-udas-grand-roadmap-to-2022/ Hustlers' march: Inside UDA's grand roadmap to 2022 ; The Star (Kenya) 25.01.2021