Tuzo za muziki MTV Afrika 2016

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tuzo za Muziki MTV Afrika 2016 zilifanyika tarehe 22 Oktoba 2016, katika Ticketpro Dome jijini Johannesburg, Afrika Kusini [1]. Ilitambua na kuwatuza wanamuziki na wafanisi walioleta athari kwa muziki wa Kiafrika na utamaduni wa vijana.[2] Sherehe ya tuzo hizo ilionyeshwa moja kwa moja kwenye MTV Base Archived 13 Julai 2013 at the Wayback Machine..  Ilisambazwa duniani kote kwenye vituo vya washirika na majukwaa ya maudhui. Hafla kilisimamiwa na Yemi Alade na Bonang Matheba. Ilitoa maonyesho kutoka Future, Yemi Alade, na wengine.

Sherehe ilidhaminiwa na Google, MTN na DStv. Ilisheherekea vipaji vya Afrika katika vipengele 18 vya tuzo. Ikiwa ni pamoja na mwanamuziki bora wakiume, mwanamuziki bora wakike,nyimbo bora na nyimbo bora ya kushirikiana. Mchango wa wasanii kutoka nchi za ureno na nchi zinazozungumza lunga ya kifaransa zilitambuliwa katika vipengele vya ubora wa Lusophone na Francophone. Vipengele vilivyoongezewa ni pamoja na tuzo za The Africa Re-imagined na Haiba ya mwaka. Waliochaguliwa walitangazwa 21 septemba Johannesburg na 2 oktoba Lagos.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tuzo za muziki MTV Afrika 2016 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.