Tonto Dikeh

Tonto Charity Dikeh (amezaliwa 9 Juni 1985) ni mwigizaji, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mfadhili wa kibinadamu wa Nigeria. [1]
Maisha Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Dikeh alizaliwa katika familia yenye watoto saba na yeye ndiye mtoto wa tatu kati ya watano. Familia yake inatoka Obio-Akpor, serikali ya mtaa (LGA) katika Jimbo la Rivers, kusini mwa Nigeria, na ni wa kabila la Ikwerre.[2][3] Akiwa na umri wa miaka mitatu, alimpoteza mama yake mzazi na kulelewa na mama yake wa kambo, ambaye naye alikuwa na watoto wawili.[4]
Dikeh alisomea uhandisi wa petrochemical katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Rivers (zamani kikijulikana kama Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jimbo la Rivers).[5]
Mnamo Septemba 2021, mchumba wake wa zamani, Prince Joseph Kpokpogri, alimshtaki yeye na Idara ya Usalama wa Taifa (DSS) kwa madai ya kutishia haki zake za msingi za binadamu.[6] Kpokpogri alidai alimuacha Tonto kwa sababu ya tabia yake ya uvutaji sigara kupita kiasi na unywaji wa pombe kupita kiasi.[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Trin, Mercy (2022-02-26). "Kayanmata: Amidst criticisms, actress Tonto Dikeh issues out a public statement". Kemi Filani News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-03-15.
- ↑ "Tonto Dikeh". Naij.com – Nigeria news. Iliwekwa mnamo 9 Februari 2017.
- ↑ "Actress Tonto Dikeh Full Biography Life And News – How Nigeria". How Nigeria. 29 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 9 Februari 2017.
- ↑ "Photos – Tonto Dikeh Shares Late Mum, Step Mother & Dad". MJ Celebrity Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-19. Iliwekwa mnamo 24 Oktoba 2016..
- ↑ "Ten things you may not know about Tonto Dikeh - Premium Times Nigeria" (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2012-10-20. Iliwekwa mnamo 28 Juni 2022.
- ↑ "Tonto Dikeh's estranged lover, Prince Kpokpogri drags DSS, actress to court over threat to fundamental rights". TonyGutsy. 22 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.
- ↑ "Your hard smoking and heavy drinking made us break-up, Kpokpogri claps back at Tonto Dikeh". Punch Newspapers (kwa American English). 2021-09-23. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2021.
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tonto Dikeh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |