Tongai Moyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tongai Moyo Tarehe 2 Machi 1968 - 15 Oktoba 2011 alikuwa mwanamuziki wa kisasa wa Zimbabwe, hujulikana kama Dhewa. alizaliwa na kukulia huko Kwekwe, alijipatia umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 kama msanii wa kujitegemea na akiwa na bendi ya Utakataka Express.[1] Nyimbo zilizofanya vizuri sana zikiwemo "Samanyemba ", " Naye", na " Muchina Muhombe " ziliongoza kwa taifa lake, umaarufu wa kikanda na kimataifa; alitoa albamu 14 katika kazi ya zaidi ya miaka ishirini.[2]

Albamu yake ya 14 na ya mwisho, Toita Basa, ilitolewa tarehe 25 Novemba 2010 na lebo ya rekodi ya Gramma Records. [3]  Albamu hiyo ilitolewa alipokuwa akitibiwa saratani, ambayo iligunduliwa mnamo 2008. Wimbo "Ndinobvuma" ulitolewa hasa kwaajili ya mapambano yake dhidi ya ugonjwa huo. [4]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]