Nenda kwa yaliyomo

The Thundermans

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Faili:Thunder 3.jpg
The Thundermens

The Thundermans ni mfululizo wa televisheni ya Marekani ambao umetengenezwa na Jed Spingarn uliofanyika kwenye Nickelodeon kuanzia Oktoba 14, 2013 hadi Mei 25, 2018.

Wahusika wa mfululizo huo ni Kira Kosarin, Jack Griffo, Addison Riecke, Diego Velazquez, Chris Tallman, Rosa Blasi, Maya Le Clark, na Dr Koloso

Mfululizo huu wa televisheni una mafunzo mengi na kuonyesha juu ya familia hii ya Thundermans ambayo si familia ya kawaida bali ni familia ya watu sita wenye nguvu za ajabu lakini baada ya kuwa saba kwa kupata mtoto mwingine, familia imekuwa ikipitia majaribu tofauti na kutumia nguvu zao za ajabu kuyavuka na kwa ushirikiano wa ndugu zao kuweza kupita majaribu hayo.kipindi hichi maarufu kimetamba juu ya mioyo ya watoto kuwapa burudani na uwezo wa kujikaza huku ukipitia magumu katika maisha huku ikiwa na vituko vya hapa na pale ikiwa katika mfululizo wa vipindi vya Nickelodeon.

Historia ya the Thundermans[hariri | hariri chanzo]

Mr.Thunderman akiwa kama mojawapo wa nyota wa kipindi hicho na utambulisho wake kama Chris Tallman kama baba wa familia yao amekuwa akipitia matitizo tofauti ili kuishi vizuri pamoja na ndugu zake na familia yake ili kuwaelekeza njia sahihi ya kutumia nguvu zao kwa ajili ya maslahi ya watu wao.

Electress akiwa kama mama wa familia ya the thundermans na utambulisho wake wa kweli kama Rosa Blasi aliye na hamu ya kuwalinda watoto wake zaidi ya chochote.

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu The Thundermans kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.