The Sixth Sense

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The Sixth Sense
Imeongozwa na M. Night Shyamalan
Imetayarishwa na Kathleen Kennedy
Frank Marshall
Barry Mendel
Imetungwa na M. Night Shyamalan
Nyota Bruce Willis
Haley Joel Osment
Toni Collette
Olivia Williams
Muziki na James Newton Howard
Sinematografi Tak Fujimoto
Imesambazwa na Buena Vista Pictures
Imetolewa tar. 6 Agosti 1999
Ina muda wa dk. Dk. 107
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu Mil. 40,000,000 za USA
Mapato yote ya filamu $672,806,292[1]

The Sixth Sense ni filamu ya kisaikolojia-kutisha ya mwaka wa 1999, ambayo imetungwa na kuongozwa na M. Night Shyamalan. Ina zungumzia hadithi kuhusu bwana mdogo Cole Sear, mwenye matatizo, kijana aliyetengwa (Haley Joel Osment) ambaye anadai ya kwamba ana uwezo wa kuona na kuzungumza na wafu, na ni kitendo sawa na kile cha mwanasaikolijia wa watoto (Bruce Willis) anayejaribu kumsaidia kijana huyo.

Filamu ilitangazwa Shyamalan akiwa kama mtunzi na mwongozaji, na ilitambulisha katika makumbi ya sinema ya hadhara ikiwa na sahihi zake, kilichokuwa maarufu zaidi katika filamu hii ni ule uwishaji wake wa utata-utata. Filamu ilipewa Tuzo sita za Academy, ikiwa kama filamu bora.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Muhtasari wa filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mwa filamu, Dk. Malcolm Crowe (Bruce Willis) mwanasaikolojia mashuhuri wa watoto, amerejea nyumbani kwake usiku mmoja akiwa na mkewe, Anna Crowe (Olivia Williams), wakiwa wanatokea katika sherehe za ugawaji wa tuzo za madaktari ambamo naye alipewa tuzo hizo akiwa kama daktari bora wa watoto.

Wawili hao wakagundua ya kwamba hawapo peke yao - Vincent Grey (Donnie Wahlberg), mgonjwa wa zamani wa Crowe, akionekana katika njia ya mlango wa kuelekea bafuni kwao akiwa na silaha huku akisema, "Sitaki kuwa naogopa tena." Grey anamlaumu Crowe kwa kushindwa kumtibia yeye, na Crowe akamtambua Vincent kama mgonjwa wake wa zamani ambaye alimtibia mara moja wakati wa utoto wake alivyokuwa akisumbuliwa na ndoto. Grey akamtandika Crowe risaidi ya tumbo, halafu baadaye akajitandika mwenyewe risasi ya kichwa. Kipande hicho kimeishia Crowe na mkewe akiwa yupo pembeni yake.

Sehemu ya pili inaonyesha Crowe anafanya kazi na kijana mwingine, mwenye umri wa miaka tisa - Cole Sear (Haley Joel Osment), mwenye hali sawa na ile ya Vincent. Crowe ikambidi ajitolee muhanga kwa mgonjwa huyu, ingawa bado alikuwa na shaka juu ya uwezo wake ni hasa baada ya kushindwa kumtibia Vincent. Baada mda mfupi, akaanza kuonekana dhahiri kuwa hashuhuriki na mkewe, ambaye baadaye mahusiano yao yakaja kupagalanyika.

Crowe alipata umanifu mkubwa kwa Cole na kisha ikatokea Cole kumweleza ya kwamba anaweza "kuona watu waliokufa." Ingawa Crowe kwa mara ya kwanza alifikiria ya kwamba Cole ana fikra potofu, lakini baadaye akaja kuamini ya kwamba anachosema Cole ni kweli na huenda ikawa Vincent alikuwa na uwezo sawa na ule wa Cole.

Aligundua hili usiku mmoja alipokuwa akilisiliza moja kati ya tepu zake za zamani, iliyorekodiwa akiwa ana mtibia Vincent, na kuweza kusikia sauti za wafu zilizokuwa zikijitetea kwa nyuma. Akamshauri Cole kwamba ina mbidi anafuta namna ya kutumia zawadi yake aliyopewa ya kuweza kuzungumza na vizuka, huenda ikawa hata kuwasaidia kazi zao ambazo hawakuzimalizia hapa duniani. Mwanzo Cole hakutaka kuusikiliza ushauri huu, kadri vizuka vinayozidi kumtisha, lakini mda mfupi akaamua kujaribu.

Mwishoni Cole akaamua kuongea na mmoja kati ya vizuka hivyo, msichana anayeumwa sana aliyeonekana chumbani kwake. Akagundua kwamba huyo msichana anaitwa Kyra Collins (Mischa Barton) na akaamua kwenda nyumbani kwao wakati wa mazishi yake. Kizuka cha Kyra kikatokea na kumpa Cole kisanduku, ambacho kinatepu ya video ndani yake na kilifichua siri nzima ya umauti wake.

Pale Cole alipompa kile sanduku baba wa Kyra, tepu ikaonyesha ya kwamba alikuwa na homa kali mno, mamake alimwekea sumu kwenye chakula, na hicho ndicho kilichopelekea umauti wa Kyra.[2] Sasa anaamini kutumia uwezo wake na zawadi aliopewa kiufanisi, baadaye Cole akaamua kumwelezea mama yake siri yake, Lynn (Toni Collette).

Ingawa mamake awali hakumwani, baada ya muda Cole akaanza kumweleza Lynn kuhusu mamake mzazi (bini yake Cole) kuna siku mmoja alikwenda kutazama tumbuizo la mwanawe wakati yupo mtoto, na Lynn hawakuwa makini na kucheza dansi hiyo kwa kfuatia mamake alikuwa nyuma ya watazamaji na kuepelekea mamake kutomwona akitumbuiza.

Pia alimpa majibu yake yote ya maswali aliouliza akiwa peke yake juu ya kaburi la mama yake. Lynn alilia sana baada ya kukubali alilosema ni la kweli. Cole pia akapatanisha ndoa ya Crowe, na kumshauri kwamba azungumze na mkewe akiwa amelala.

Imani yake mwenyewe sasa imerejea kwa majibu ya kufaulu tatizo la Cole, Crowe akarudi zake nyumbani, ambamo alimkuta mkewe amelala kwenye kochi akiwa na mikanda miwili ya video ya harusi ikiwa inalia kwa nyuma, na sio kwa mara ya kwanza. Akiwa amealala, mkonoi wa Anna imetoa pete ya ndoa ya Malcolm (ambayo baada ya muda mfupi akagundua ya kwamba alikuwa hakuivaa).

Kwa kufuata ushari wa Cole, Crowe kaamua kurudi nyumbani, na kuzungumza na mkewe huku akimweleza ya kwamba, "mkewe hakuwa wa pili katika mambo yake," na kwa hiyo ana mpenda mkewe. Akamwacha aendelee na maisha yake mwenyewe, na yu huru kuishi katika dunia ya tofauti na ile ya kawaida ya watu wanaoshi. Filamu inaishia kwa kipande kifupi cha sehemu ya harusi kinachopotea taratiibu kwenye kiza.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]