The Puppy Episode
"The Puppy Episode" | |
---|---|
Sehemu ya Ellen | |
"Susan...I'm gay." Ellen Morgan anafunguka. | |
Sehemu ya. | Msimu 4 Sehemu 22/23 |
Imetungwa na | Ellen DeGeneres |
Imeongozwa na | Gil Junger |
Tarehe halisi ya kurushwa | Aprili 30, 1997 |
Waigizaji wageni | |
| |
Msimu 4 sehemu
Orodha ya sehemu za Ellen |
"The Puppy Episode" ni kisa chenye sehemu mbili ya ucheshi mfululizo wa televisheni Ellen. Kisa hiki kimejikita zaidi katika kumwelezea muhusika mkuu Ellen Morgan katika kutambua kwake kama yeye ni mpenzi wa mahusiano ya jinsia moja na kufunguka kwake kwa hadhira. Ilikuwa kisa cha 22 na 23 katika mfululizo wa msimu wa nne. Kisa hiki kilitungwa na nyota wa mfululizo huu Bi. Ellen DeGeneres akiwa pamoja na Mark Driscoll, Tracy Newman, Dava Savel na Jonathan Stark na kuongozwa na Gil Junger. Kisa kilirushwa kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha TV cha ABC mnamo tarehe 30 Aprili, 1997. Jina la kisa lilitumika kama jina la siri kwa ajili kufunguka kwa Ellen na kuweka ule usiri mkubwa kabisa wa kisa kizima.
DeGeneres alianza kujadiliana na ABC mnamo 1996 kumfanya Morgan ajitokeze kama ni mpenda mahusiano ya jinsia moja. Wakati majibu ya makubaliano yalivyotoka tu, DeGeneres alijikuta katika tafakuri nzito juu yake mwenyewe na hata uhusika wake wa kufunguka kama shoga. Pamoja na DeGeneres mwenyewe kuwa anagusiagusia juu ya uhusika wake katika kufunguka akiwa ndani ya TV na nje ya TV na ndani ya kipindi, duru zilithibitika pale kisa kilivyoenda kuzalishwa mnamo mwezi wa Machi 1997.
Licha ya vitisho kutoka kwa wadhamini na makundi ya kidini, "The Puppy Episode" ilipata mafanikio makubwa sana ya kitahakiki, ilishinda tuzo chungunzima na ikawa moja kati ya kitu kikubwa cha kitamaduni. Hata hivyo, DeGeneres na kipindi chake wakapondwa sana kwa kuwa "kishoga mno"; mfululizo ukaghairishwa baada ya msimu mmoja na mwigizaji mwalikwa Laura Dern na Ellen wote wakaingia katika misukosuko mizito ya kazi ya uigizaji.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Ellen anaenda mtoko na rafiki yake wa kitambo, Richard, mwandishi wa habari aliye mjini kwa ajili ya habari fulani. Matayarishaji wake, Susan, anaungana nao kwa ajili ya kifunga mlo. Susan na Ellen wanaelewana mno licha ya ugeni wao katika kujuana. Ellen anarudi katika chumba cha hoteli cha Richard. Richard anamtakia mambo ya kimapenzi Ellen, anajionea tabu, anaondoka. Anakumbana na Susan ukumbini na kurudi naye chumbani kwake. Wanaendelea kufurahia maisha hadi hapo Susan anapomwambia Ellen ya kwamba yeye ni mpenda mahusiano ya jinsia moja na anafikiri Ellen huenda akawa hivyo pia. Ellen anakana hilo na kusema ati Susan anajaribu kumwingiza kundini. Susan akatia kijembe cha utani ati atawapigia simu "makao makuu ya taifa" na kuwafahamisha ya kwamba Ellen kakimbia. Ellen mwenye huzuni anaondoka chumbani kwa Susan na kurudi chumbani kwa Richard, kwa azimio la kwenda kufanya naye mapenzi ili kujithibitishia ya kwamba yeye si mshabiki wa mapenzi ya jinsia moja.
Siku iliyofuata, Ellen anawaeleza marafiki zake wa duka la vitabu ya kwamba alipata penzi kabambe na Richard. Anamwelezea ukweli mtaalamu wake wa matibabu, ya kwamba ameshindwa kufanya mapenzi na Richard. Ellen anasikitika ya kwamba anamtaka mtu ambaye anaendana naye. Mtabibu wake anamwuliza kama amewahi kukutana na mtu anayeendana naye Ellen anajibu, "Susan."
Ujumbe kutoka kwa Richard ya kwamba anaondoka mjini pale kabla ya muda unamkurupua Ellen kukimbilia uwanja wa ndege kumwona Susan. Ellen anamwambia Susan kwamba alikuwa sahihi lakini anashindwa kulitamka hilo neno. Hatimaye, Ellen anaweza kusema, "Mimi ni shoga," bila kuwa makini anajikuta kutangaza kupitia mifumo ya utangazaji ya umma ya uwanja wa ndege. Ellen anadhani ya kwamba Susan ataondoka na Richard kumbe hali halisi Susan atabaki mjini kwa siku kadhaa zaidi.
Ellen anaota akifanya manunuzi ya vitu vya nyumbani. Huko manunuzini, anapewa ofa maalumu katika matikitimaji, na kupewa ofa nyengine kemukemu. Anajadiliana na mtabibu wake na kutambua ya kwamba alikuwa akizibana hisia zake za kimapenzi kwa muda mrefu sana. Mtabibu wake anamtia hamasa ya kufunguka juu ya hali yake kwa marafiki zake lakini Ellen anaingia wasiwasi wa kutokubalika mbele ya jamii.
Ellen anawaita marafiki zake kwa minajili ya kuwafungukia. Kabla hawajafika, anamfungukia jirani yake ambaye ni shoga Peter. Wakati kila mmoja amewasili, Ellen anasita kuwambia ukweli lakini Peter anamsaidia kuwaambia kama Ellen ni shoga. Ellen anathibitisha ya kwamba kuwa kweli yeye ni shoga na marafiki zake wote wanamwunga mkono, ijapokuwa rafiki yake mmoja aitwaye Paige anasita.
Siku iliyofuata Ellen na Susan wapo katika duka la vitabu. Susan anamweleza Ellen ya kwamba anampenda lakini yupo katika mahusiano ya muda mrefu na mtu mwingine. Ellen anavunjika moyo na Susan anaondoka. Katika kumpoza, marafiki zake wanatoka naye hadi katika duka la kahawa. Wakiwa huko, Ellen anadhani muhudumu wa pale anamfanyia ubobishi yeye badala yake ukamhusu Paige badala ya yeye.
Mwishoni mwa kisa, Susan anampeleka Ellen kwa Melissa Etheridge, ambaye alimthibitishia Ellen kwamba yeye ni shoga, na baada ya kumaliza kusaini mikataba maalumu, Susan akatoa shereheko la nguvu.
Utayarishaji
[hariri | hariri chanzo]Mapokezi
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Castañeda, Laura; Campbell, Shannon B. (2005). News and Sexuality: Media Portraits of Diversity. Thousand Oaks, CA: SAGE. ISBN 1-4129-0999-6.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help); Unknown parameter|last-author-amp=
ignored (|name-list-style=
suggested) (help) - Capsuto, Steven (2000). Alternate Channels: The Uncensored Story of Gay and Lesbian Images on Radio and Television. New York: Ballantine Books. ISBN 0-345-41243-5.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Ehrenstein, David (1998). Open Secret (Gay Hollywood 1928–1998). New York: William Morrow. ISBN 0-688-15317-8.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Johnson, Victoria E. (2008). Heartland TV: Prime Time Television and the Struggle for U.S. Identity. New York: NYU Press. ISBN 0-8147-4293-9.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Marchessault, Janine; Sawchuk, Kim (2000). Wild Science: Reading Feminism, Medicine, and the Media. London: Routledge. ISBN 0-415-20431-3.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help); Unknown parameter|last-author-amp=
ignored (|name-list-style=
suggested) (help) - Tracy, Kathleen (2005). Ellen: The Real Story of Ellen DeGeneres. New York: Kensington. ISBN 0-7860-1750-3.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Tropiano, Stephen (2002). The Prime Time Closet: A History of Gays and Lesbians on TV. New York: Applause Theatre & Cinema Books. ISBN 1-55783-557-8.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)