Ellen DeGeneres

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ellen DeGeneres
PortiadeRossiEllenDeGeneresHWOFSept2012.jpg
Portia de Rossi na DeGeneres mnamo Septemba 2012
Amezaliwa 26 Januari 1958 (1958-01-26) (umri 65)
Metairie, Louisiana, US

Ellen Lee DeGeneres (amezaliwa tar. 26 Januari 1958) ni mwigizaji wa filamu na mchekeshaji kutoka nchini Marekani. Maarufu kwa kipindi chake cha mazungumzo kinachokwenda kwa jina la Ellen Show. Ellen ni mama wa kwanza katika tasnia ya vipindi vya mazungumzo kujitokeza hadharani na kusema kwamba yeye anapenda mahusiano ya jinsia moja. Hatua hii ilipelekea kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa anaishi na baba yake mzazi kwa kuhofia kuambukiza tabia hiyo mbaya kwa ndugu zake wa kike wengine wawili waliozaliwa baba mmoja lakini mama tofauti. Kipindi hiki mzee wake alikuwa ameoa mke mwengine na walibahatika kupata wawili na mke huyo. Wengi walihisi huenda mama wa kufikia alitia fitina kati yake na baba yake ili aondoke, jambo ambalo lilimuumiza Ellen lakini hatimaye aliyamaliza hayo.[1] [2]

Kwa mara ya kwanza aliuonesha umma wa watu wa Marekani kama yeye ni mpenzi wa mahusiano ya jinsia moja ilikuwa katika mfululizo wa TV wa Ellen uliokuwa unarushwa na TV ya ABC katika kisa maarufu cha "The Puppy Episode" kilichorushwa hewani mnamo tarehe 30 Aprili 1997. Kisa hicho kinamuelezea Ellen Morgan ana mahusiano na mwanamke mwenzake ambaye wakati huo alikuwa Laura Dern kwa pamoja walipata tabu sana katika kazi zao za uigizaji, kazi zilipotea na wakaanza moja. Walitengwa na watu wengi, makundi mbalimbali wanaopinga mahusiano ya jinsia moja. Ilichukua muda sana hadi Ellen na mwenzake kurudi tena katika soko. Mwezi wa Agosti 2008, baada ya sheria ya kukinga ndoa za jinsia moja kuondolewa huko jijini Los Angeles, Ellen na Portia walioana rasmi kuwa mke na mke.[3]

Mbali na vipindi vya TV na kadhalika, Ellen vilevile ni mwandishi wa vitabu mbalimbali. Hii ni sehemu ya baadhi ya vitabu vyake;


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. (2006) News and sexuality : media portraits of diversity, Castañeda, Laura, 1963-, Campbell, Shannon B., Casta๑eda, Laura, 1963-, Thousand Oaks, Calif.: Sage Publications. ISBN 1412909988. OCLC 59881923. 
  2. Steven., Capsuto, (2000). Alternate channels : the uncensored story of gay and lesbian images on radio and television, 1st, New York, NY: Ballantine Books. ISBN 0345412435. OCLC 44596808. 
  3. "Ellen and Portia's Love Story", Us Weekly (in en-US), 2012-01-26, retrieved 2018-09-30 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Us-actor.svg Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ellen DeGeneres kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.