Tepu ya sumaku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanda ya sauti

Tepu ya sumaku (vilevile mkanda wa sumaku, kutoka Kiingereza magnetic tape) ni jina la kutaja mkanda mrefu na mwembamba wa plastiki ambao umepakazwa malighafi ya kisumaku juu yake. Karibu tepu zote za kurekodia, aidha iwe ya sauti au video, au kwa ajili ya kuhifadhia data za kompyuta, zina usumaku ndani yake.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tepu za sumaku ziligunduliwa kwa mara ya kwanza na mtaalamu wa mambo ya sauti wa Kijerumani Fritz Pfleumer mnamo 1928 nchini Ujerumani. Uvumbuzi wa Pfleumer ulitumia iron oxide (Fe2O3) ungaunga alioupakaa katika ukanda wa karatasi.

Tepu za sumaku zimekuwa zikitumika kuhifadhia data mbalimbali kwa zaidi ya miaka 50. Hadi sasa, matepu ya kibao ya kisasa yamepata kutengenezwa. Leo hii, teknolojia nyingine kadha wa kadha kama vile CD au DVD zinachukua nafasi ya tepu ya sumaku. Hata hivyo, pamoja na ugunduzi wa kiteknolojia kutokea, bado matumizi ya tepu za sumaku yanaendelea.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.