Kanda (kifaa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kanda ya sauti)
Kanda ya kawaida ya sauti.

Kanda (kwa Kiingereza: audiocassette) ni aina ya kanda (kaseti) ambayo inatumika kuhifadhi sauti na muziki. Hii inaweza kutumika kwa "kicheza kanda" au "tanakali kanda". Kanda zinahifadhi sauti katika tepu ya sumaku ambayo imeviringishwa katika rola mbili za kanda.

Kanda sanifu ya kwanza iligunduliwa mwaka 1962 na kampuni ya Philips. Wao waliita "Compact Cassette". Wakati huo zinapoanza (miaka ya 1960) kanda-kaseti na vifaa vyake vya kurekodia havikuwa bora sana. Lakini ilipofika miaka ya 1970 kila mtu alipenda kusikiliza muziki kupitia kaseti na hivyo polepole teknolojia ikawa poa zaidi.

Ilipofika miaka ya 1980, zikazidi kuvuma na ubora ukaongezeka maradufu. Katika kufanikisha hili, kampuni ya Sony ikatengeneza Walkman na hapo ndipo palipozidisha soko la kanda.

Kwa kufuatia matumizi makubwa ya CD, matumizi ya kanda yakaanza kufifia. Mwaka wa 2011 hata Kamusi ya Kiingereza ya Oxford iliondoa neno "cassette tape" katika toleo dogo la vitabu vyake.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. David Moye. "Oxford Dictionary Removes 'Cassette Tape,' Gets Sound Lashing From Audiophiles", 22 October 2011. Retrieved on 28 July 2013. 
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.