Tamasha la Ariginya
Tamasha la Ariginya ni tamasha maarufu linalosherehekewa katika moja ya miji ya jimbo la Ondo iitwayo Ikare Akoko. Kulingana na lahaja na jinsi ya kutamka, wengine wanaliita Aringinya. Tamasha hili linadaiwa kuwa mojawapo ya tamasha la kiasili la zamani zaidi lililosherehekewa katika mji huu tangu kuanzishwa kwake. Ikare-Akoko ni mji mmoja ulipo katika eneo la kusini-magharibi mwa Nigeria, na katika eneo la Waya.[1] Tamasha hili ni moja ya tamasha nyingi zinazoadhimisha usafi na mapenzi kati ya wanawake, kwani jimbo la Waya linajulikana kwa thamani na umuhimu wake kuhusu ustaarabu na unadhifu.[2][3] Tamasha hili husaidia kuboresha mtazamo wa heshima na usafi pamoja na thamani ya mwanamke kubaki safi na mnyenyekevu hadi wakati wa ndoa na kwa mume wake pekee. Hii imeongeza kiwango cha ustaarabu katika mji huo kwa kuwa wasichana wadogo wanajua thamani ya usafi wao na kwamba sifa kubwa za mwanamke ni ubikira wake, ambayo pia ni njia ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia na dhuluma.[4][5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Ikare | Nigeria". Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Yetunde A, Aluko; Oluwasegun, Onobanjo; Nurudeen, Alliyu (1 Juni 2011). "The Centrality of Women in Moral Teaching in Yoruba Family System". The Nigerian Journal of Sociology and Anthropology. 9. doi:10.36108/NJSA/1102/90(0120). ISSN 0331-4111. S2CID 227092325.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ariginya Festival, Festivals And Carnivals In Ondo State :: Nigeria Information & Guide". www.nigeriagalleria.com. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Aringinya festival: Celebrating Ikare-Akoko's date with fertility, chastity". Tribune Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). 3 Julai 2018. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ariginya Festival, Festivals And Carnivals In Ondo State :: Nigeria Information & Guide". www.nigeriagalleria.com. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tamasha la Ariginya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |