Nenda kwa yaliyomo

Talmud

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukurasa wa Talmud: Chanzo cha kitabu cha „Berakhot“. Katikati iko Mishna na Gemara (kuanzia mstari wa 14), upande wa kulia mafundisho ya Rabbi Rashi juu ya sehemu hii, upande wa kushoto maelezo na mafundisho ya wengine

Talmud (Kiebrania: תלמוד, talmūd "mafunzo") ni maandiko muhimu katika dini ya Uyahudi.

Ni mkusanyo wa maandiko mbalimbali yaliyopangwa katika sehemu kubwa mbili ambayo ni Mishna na Gemara.

Mishna ni sehemu ya kale iliyokusanywa na kuandikwa mnamo karne ya 2 BK ikiwa mkusanyo wa sheria za kimdomo za Uyahudi. Kwa imani ya Kiyahudi sheria hizi zilikuwa sehemu ya Torati iliyotolewa na Mungu kwa Musa kimdomo kule mlima Sinai. Kufuatana na imani hiyo sheria hizo zilipitishwa kutoka kizazi hata kizazi cha wataalamu. Wakati elimu ya Uyahudi ilipungua nchini Palestina-Israeli baada ya kuharibiwa kwa hekalu la Yerusalemu wataalamu walianza kuandika mapokeo hayo kwa lugha ya Kiebrania wakaiita Mishna. Hiyo Mishna ina pia maelezo juu ya maana ya Tanakh au mkusanyo wa mawazo na mafundisho juu ya Biblia ya Kiebrania.

Gemara ni sehemu ya pili ni mkusanyo wa maandiko ya baadaye ambamo wataalamu walijadiliana maswali yaliyotokana na Mishna na maswali kutokana na Mishna, Torati na maisha halisi. Katika Gemara tunaona mawazo mengi yanayopingana kwa sababu wakusanyaji wa Talmud walijitahidi kukusanya mapokeo mapana yenye mawazo na mafundisho mbalimbali.

Kuna matoleo makubwa mawili ya Talmud: 1 ni Talmudi ya Babeli na nyingine Talmudi ya Yerusalemu (au: ya Palestina). Talmudi ya Babeli ilikusanywa huko Irak ambako Wayahudi wengi waliishi katika Milki ya Uajemi; Talmudi ya Palestina ilikusanywa katika nchi ya Israeli-Palestina. Zote mbili ni sawa kuhusu Mishna lakini kuna tofauti katika Gemara. Kwa jumla Talmudi ya Babeli huheshimiwa zaidi.

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Talmud kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.