Nenda kwa yaliyomo

Taff B.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Taff B
Kutoka kushoto: Afisa Mtendaji Mkuu wa Bongo Radio Ndugu Hassan JN a.k.a Geeque akiwa na Taff B.
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaBrian Haule
Pia anajulikana kamaNgomaNagwa
Amezaliwa16 Mei 1978 (1978-05-16) (umri 46)
Ilala, Dar es Salaam, Tanzania.
Kazi yakeMtangazaji, mtunzi, rapa
AlaKurap
Miaka ya kazi1993-hadi sasa
Ameshirikiana naProfessor Jay
John Mahundi

Brian Haule (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Taff B au lile la kimtandao zaidi Ngomanagwa; alizaliwa Ilala Bungoni/Sharif Shamba, Dar es Salaam, 16 Mei 1978) ni rapa, mtangazaji wa redio ya mtandaoni (Bongo Radio) na mdau mkubwa wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania.

Huyu ni ndugu wa baba mkubwa na mdogo wa Professor Jay.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]
Kutoka kushoto: Nigga Jay, Walter Haule na mwisho kabisa Brian Haule au NgomaNagwa - nyumbani kwa kina Jay Kimara, Dar es Salaam mnamo 1992.

Haule alizaliwa tarehe 16 Mei, 1978 huko jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukulia Ilala Bungoni/Sharif Shamba. Alisoma Shule ya Msingi Olympio na kiasi katika shule ya Msingi Mlimani wakati huo alikuwa akiishi na mama yake mzazi huko Sinza. Aliendelea na elimu ya secondari kuanzia kidato cha kwanza 1 Bagamoyo Sec, kidato cha 2-4 Kibaha Sec School na kufika mwaka 1996 akawa amemaliza. Elimu ya juu, yaani, kidato cha 5-6 alisoma Kampala 1997-1999. Mnamo mwaka 2001 alifanya Associate Degree of Business Admin (DMACC). Na sasa katika kujiongezea elemu anachukua Shahada ya Business Information System katika Shule hiyo hiyo.. Hapo awali, alisimama kabisa na masuala ya shule. Lakini kwa sasa anasoma huku anafanya kazi.

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]
Taff B, 1995 akishika kipaza sauti.

Kwa upande wa muziki, alianza kujishuhulisha nao tangu 1993 - 2002. Hapo awali kwenye 1993 alikuwa akijirusha na ndugu yake Nigga Jay ambaye alikuwa na kundi zima la Pyscho Tak ambalo lilikuwa likiongozwa na Badi Sangu. Pia alikuwa na ukaribu na kaka yake mkubwa ambaye ni Julius Haule almaarufu kama Mr Teacher. Mwaka wa 1995-96 waliunda Kundi la KNT Squad ambalo lilikuwa na wasanii watatu, "K" Killa B, "N" Nigga J na "T'" Taff B. Walifanikiwa kurekodi wimbo mmoja ulioitwa "Right Stuff" bahati mbaya huu wimbo walipoteza nakala yake kuu ya kuhifadhia. Mwaka 1997 yeye na Jay wakaunda Underground Shadow Warriors. na Killa B akaunda kundi la mtaani kwao Kimara lililoitwa Imeditaiton Kingdom. Jay na Taff walibahatika kupanda katika majukwaa kibao ikiwa ni pamoja na Korean Culture, Pool Side na kumbi nyingine chungu mzima. 1997 wakarekodi wimbo mmoja ambao Jay alishiriki kwenye kiitikio na kifungio ulioitwa "Rap ndo Yenyewe" katika studio za Soundcrafters chini ya Producer Henrico. 1998 wakarekodi Fascinating Rhymes ambao ulitayarishwa na Papa Luv aka Dj Boniluv. Mwaka 2000 akarekodi Dereva Mchovu na ndugu yake upande wa mama kwa Master Jay na Boaz Kapaya almaarufu Diz K. Mdundo wa dereva Mchovu uliandaliwa na Prof Ludigo hapo hapo kwa Master Jay wakati Mdundo wa "Ndugu upande wa mama" ulitayarishwa na John Mahundi. Diz K na Taff B walirekodi nyimbo hizo mbili muda mmoja na kundi la Hard Blasters. Wakati huo walikuwa wanarekodi albamu yao ya Funga Kazi. Prof Jay alikuwa ndio kajiunga rasmi 1999 na HBC baada ya Chuzi Limekubali kufanya vizuri sana katika vituo vya Radio. Wimbo wa mwisho ambao Taff B aliweza kurekodi akiwa Tanzania ulikuwa ni Bado "Nakutesa Remix" ya Soggy Doggy Anter katika studio ya Bongo Records kabla ya kuondokea na kuelekea nchini Marekani mnamo Disemba, 2000. Akiwa nchini Marekani, amefanya kazi nyingi sana na mtayarishaji John Mahundi baye pia ni binamu yake wa damu. Bahati mbaya, kazi nyingi zilipotea baada ya kompyuta yake kuharibika ghafla. Alitengenza kama nyimbo 30 hivi na wasanii mbalimbali. Ambazo zimebaki kama mfano-awali hazizidi hata 10 katika Maktaba yake.

Mahusiano yake na makundi mengine

[hariri | hariri chanzo]

Moja ya makundi ambayo alikuwa anashinda nayo au anajishuhulisha nayo kwa sana ni pamoja na Pyscho Tak, Hard Blasters na Imeditation Kingdom, Ugly Faces na TGK Unit. lakini vilevile alikuwa ana mahusiano mazuri sana na wasanii wa makundi mengine kama vile akina GWM, LWP na wasanii wengine wengi. Msanii Complex alisoma nae High School Kampala na jina la Complex alimpa yeye. Wakati huo alikuwa hana jina la kisanii na jina lake la kuzaliwa ni Simon Sayi, yeye sasa akampachika jina la Complex S kabla hawajapanda kwenye mashindano ya Kurap Club Silk huko mjini Kampala, Uganda. Katika shindano hilo, akajichukulia ushindi wa Kwanza mara 3 mfululizo. Baadaye Complex akahamia na kurudia mwaka wa Masomo Tanga. Huko nako akatoa herufi moja S na kubaki na Complex peke yake na kuendeleza shughuli zake za Muziki.

Throwback Monday na maktaba ya muziki wa hip-hop wa 1990

[hariri | hariri chanzo]

Hapo 2010 Hassan JN, alijaribu kumwambia Haule kama kipindi cha muziki wa zamani wa hip hop katika redio yake. Lakini hakuweza kwa kipindi hiko, akachomoa mpango huo wa kuwa mwendesha kipindi. Katika harakati zake za kupiga soga juu ya muziki na vijana ambao wengi wamezaliwa miaka ya 1990 hawajui wapi ulipotoka, ndipo alipoamua kuzikusanya na kutunza nyimbo za miaka ya 1990 na nyingine za miaka ya 2001-2006 ya miziki ya kibongo tayari kwa ajili ya kipindi cha Bongo Radio. Pia amekusanya Sehemu kubwa ya nyimbo hizo alikuwa anatumiwa na DJ Steve B kwa mfumo wa CD ama data files. Mwaka wa 2012 Hassan alikamkumbusha nia yake yeye ya kufanya kipindi, kwa vile tayari alikuwa ana vitendea kazi, hakuwa na budi kulianzishwa gurudumu hilo mnamo Disemba 2012. Mpaka leo bado anapiga kipindi hiko. Mwaka uliofuata, yaani, 2013, akajiunganisha na wasanii wengine wengi tu ili aweze kupata nyimbo za miaka ya 1990 ikiwa ni pamoja na Meneja wa kundi la vijana toka Arusha Xplastaz Jumanne Thomas ili kukuza maktaba yake. Pia amekusanya miziki ya Hip-hop, R&B, Reggea, Taarabu, Zilipendwa pamoja na aina nyingi tofauti. Hadi sasa kipindi kinafanyika kila siku ya Jumatatu kuzirusha katika izaa zake katika mitandao ya kuhifadhia sauti. Tangu aanza kazi hii, amekuwa wa kwanza kutaka kuwa na kila wimbo wa miaka ya 1990 ukiachia mbali Dola Soul na Jumanne Thomas.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Taff B. kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.