Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Nigeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Nigeria (kwa Kiingereza: Cocoa Research Institute of Nigeria; kifupi: CRIN) katika Jimbo la Oyo, Nigeria, ni taasisi ya utafiti wa kakao iliyoanzishwa na Serikali ya Shirikisho la Nigeria kupitia Sheria ya Taasisi ya Utafiti ya Nigeria ya 1964. [1] [2] Sheria hiyo ilianzisha taasisi za utafiti wa kakao, mawese, kahawa na kola.

Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Naigeria ilianzishwa ili kukuza na kuboresha uzalishaji ya kakao na bidhaa yake inchini Nigeria na kimataifa. Awali Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Nigeria ilikua sehemu ya Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Afrika Magharibi yenye makao yake makuu Tafo, Ghana.

Kakao na bidhaa yake hutumika kama chanzo cha mapato na ajira kwa wakulima katika majimbo yanayozalisha kakao ya Nigeria.

Kazi kuu ya Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Nigeria ni kufanya utafiti wa ubora wa juu katika kakao, kola, na kahawa na pia kutoa vifaa vya kufundishia na kutafiti na bidhaa hizi za kilimo.

Utafiti[hariri | hariri chanzo]

Taasisi ya Utafiti wa Kakao ya Nigeria ilitoa aina mpya za kakao mnamo 2013. [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Allen Kent, Harold Lancour and Jay E. Daily (1 February 1977). Encyclopedia of Library and Information Science: Volume 20 - Nigeria: Libraries in to Oregon State University Library. CRC Press. uk. 29. ISBN 978-0-8247-2020-9.  Check date values in: |date= (help)
  2. "History of Cocoa Research Institute of Nigeria (CRIN)". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 September 2014. Iliwekwa mnamo 25 September 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "Cocoa Research Institute of Nigeria (CRIN) Archives - Independent Television/Radio". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 November 2016. Iliwekwa mnamo 31 October 2016.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)