Nenda kwa yaliyomo

Ténès

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ténès (kwa lugha ya Kiberber: Tinas) ni mji wa Algeria unaopatikana kilomita 200 kutoka mji mkuu, Algiers, na una idadi ya watu wapatao 35,000.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Maghofu yanayopatikana Ténès.

Ténès ilikuwa bandari ya Wafoinike kabla ya karne ya 8 kabla ya Kristo. Kama makoloni mengine ya Wafoinike, iliangukia katika milki ya Carthage katika karne ya 6 kabla ya Kristo, na kwa Waroma katika vita vya uhaini. Jina lake la uhaini ulikuwa katika lugha ya kilatini kama Cartennae.[1] Mji ulichukuliwa na Waroma na kuwa koloni ya Waroma. Ilitekwa nyara na ufalme wa Vandal katika ushindi wa dhidi ya Waroma kaskazini mwa Afrika. Ilipotea isipokuwa ngome ya kale iliyosalia.

Zama za kati za Ténès zilitokana na uislamu wa kihispania wa karne ya 9; Al-Bakri alitaja mwaka 875 au 876. Walianzisha makao yao katika makazi yao ya hapo awali. Waliwakaribisha wakazi kutoka Elvira, Hispania na Murcia ila wengi waliondoka kutokana na mlipuko wa homa miongoni mwa wakazi wapya. Mji uliimarika japokuwa hali ya hewa haikuwa nzuri kwani udongo haukuwa na rutuba na hivyo kuathiri kilimo cha matunda.

Kwa sasa

[hariri | hariri chanzo]

Kwa wakati huu, Ténès ni mji mdogo wa kitalii wenye hoteli ndogo tano, hospitali mbili, nyumba ya makumbusho, bandari na mnara wa taa. Una maeneo kuhusu mambo ya kale kama vile makaburi ya waroma na Wafoinike, mapango ya kihistoria ya Sidi Merouane, msikiti wa Sidi Ahmed Boumaza, Bab El Bahr, Notre Dame de Ténès, mizinga ya Kifaransa na mengine mengi.

  1. Playfair, Robert Lambert (1891). Handbook for Travellers in Algeria and Tunis. J. Murray. ku. 246–247. Iliwekwa mnamo 18 Machi 2018.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ténès kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.