Mlangobahari wa Magellan
Mlangobahari wa Magellan (kwa Kiingereza: Strait of Magellan) ni nafasi ya kupita kwa chombo cha bahari kutoka Atlantiki hadi Bahari Pasifiki bila kuvuka Rasi ya Hoorn.
Ni njia nyembamba ya maji inayopita kati ya Amerika Kusini bara na Tierra del Fuego (Nchi ya moto). Pwani zake ni za Argentina upande wa kaskazini na Chile upande wa kusini. Nchi hizo mbili zilivutana kwa muda mrefu ni nani anayestahili kusimamia mlangobahari huu, sasa iko chini ya Chile.
Jina lilitolewa kwa heshima ya nahodha na mpelelezi Mreno Ferdinand Magellan aliyepita hapa mara ya kwanza.
Si njia nyepesi kwa meli na jahazi maana kuna dhoruba za mara kwa mara na ukungu mwingi.
Picha
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- The first map made of the Strait of Magellan. It was made in 1520
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|