Nenda kwa yaliyomo

Steve Abbley

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Steve Abbley (alizaliwa Liverpool, 19 Machi 1957) ni mchezaji wa zamani wa kandanda aliyetumikia maisha yake mengi ya kandanda kwenye ligi za chini, Swindon Town ndiyo timu iliyomtambulisha kama mchezaji wa kulipwa. Kwa sasa ni mwenyekiti wa Cirencester Town.[1]

Stephen George Abbley alianza maisha yake kandanda kwenye ligi ya chini kwenye klabu ya Parks F.C na baadaye alijiunga na Swindon Town akiwa na umri wa miaka 22 mnamo mwezi wa 10 mwaka 1979.

Abbley alikuwa akicheza katika nafasi ya beki wa kulia mda mwingine kama beki wa kushoto. Alipitia kipindi kigumu Hata hivyo, Abbbley alijitahidi kuingia katika kikosi cha kwanza cha Swindon.

Msimu wa kwanza alicheza michezo mitano pekee. Majukumu yalikuja  badae kwenye mchezo waliopoteza 2-0 dhidi ya Blackburn Rovers mwezi wa 3 mwaka 1980.

Alipata ushindi wake wa kwanza 3-0 dhidi ya Gillingham, Abbley na kapteni wa Manchester United Steve Bruce walitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliokuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya juu.[2]

Msimu wa pili wa Abbley akiwa Swindon alicheza mechi tatu pekee kwenye kikosi cha kwanza.[3]

  1. https://web.archive.org/web/20080703160202/http://www.sportssolutionsgb.co.uk/pdfs/Cirencester%20case%20study.pdf
  2. https://web.archive.org/web/20071006064709/http://www.swindon-town-fc.co.uk/MatchReport.asp?MatchID=19800142
  3. http://www.swindon-town-fc.co.uk/PlayingRecord.asp?PersonID=ABBLEYST&Season=1980-1981