Simi (mwimbaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simi
Jina Kamili Simisola Bolatito Kosoko
Jina la kisanii Simi
Nchi Nigeria
Alizaliwa 19 Aprili 1988
Aina ya muziki Afropop, Soul
Kazi yake Mwanamuziki
Miaka ya kazi 2006 - hadi leo

Simisola Bolatito Kosoko (née Ogunleye, anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Simi; alizaliwa Ojuelegba, kitongoji cha Surulere, Jimbo la Lagos, 19 Aprili, 1988) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji wa Nigeria.[1]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Simi ni mtoto wa mwisho kati ya wanne. Katika mahojiano na Juliet Ebirim wa gazeti la Vanguard, Simi alibainisha kwamba wazazi wake walitengana alipokuwa na umri wa miaka 9. Pia alifichua yakuwa alikuwa kama tomboy katika umri huo.[2]

Alianza kazi yake kama mwimbaji wa nyimbo za injili, akitoa albamu yake ya kwanza mnamo 2008, iliyoitwa Ogaju.[3] Pia alicheza kama mmoja wa waamuzi wakuu katika msimu wa 7 wa kipindi cha Nigerian idol Tv mnamo 2022.[4]

Alipata kutambuliwa na umma mwaka wa 2014 baada ya kuachia "Tiff", wimbo ambao uliteuliwa kwa Wimbo Bora Mbadala katika The Headies 2015. Simi alisaini mkataba wa rekodi na X3M Music mwaka wa 2014, lakini aliondoka kwenye lebo hiyo Mei 2019 kufuatia kumalizika kwa mkataba wake. Alitoa albamu yake ya pili ya studio Simisola mnamo Septemba 8, 2017. Albamu yake ya tatu ya studio Omo Charlie Champagne, Vol. 1 ilitolewa sanjari na siku yake ya kuzaliwa ya thelathini na moja mnamo Aprili 19, 2019. Alizindua lebo yake ya rekodi ya Studio Brat mnamo Juni 2019.[5]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu za studio

  • Ogaju (2008)
  • Chemistry (with Falz) (2016)
  • Simisola (2017)
  • Omo Charlie Champagne, Vol. 1 (2019)
  • To Be Honest (2022)

EPs

  • Restless (2014)
  • Restless II (2020)

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mokalik (2019)[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "How Old is the ‘Duduke’ Singer and What Is Her Net Worth in 2022?". Buzz Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-19. 
  2. "Why I do love songs – Simi". Vanguard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2016-03-14. 
  3. "I started with gospel music – SImi". National Dailyng (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2016-04-21. 
  4. "Nigeria: Even the Silliest Things Inspire Me - Simi". All Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2016-04-21. 
  5. "Simi launches her record company, Studio Brat". Pulse.ng (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-06-20. 
  6. "5 things you should know about Kunle Afolayan’s new movie, ‘Mokalik’". Pulse.ng (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-03-28. 
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simi (mwimbaji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.