Simeon Mulama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simeon Mulama
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
1997Mathare United
1998AFC Leopards
1999–2001Mathare United
2001–2002Ismaily
2002–2005Park University
2007Skellefteå FF
2009–Mathare United
Timu ya Taifa ya Kandanda
2000–2001Kenya11(1)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 3 August 2011.
† Appearances (Goals).

Simeon Mulama (alizaliwa mnamo 6 Agosti 1980 katika eneo la Huruma, katika mji mkuu wa Nairobi) ni mwanakandanda wa kitaifa wa Kenya aliyestaafu mwaka wa 2009.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Mulama alianza kucheza akiwa katika Shule ya Msingi ya Dr Aggrey. Kisha alijiunga na Shule ya Upili ya Kakamega na baadaye Shule ya Upili ya Kisii. Mwaka wa 1996 aliichezea timu ya ligi ya mkoa ya Gusii Mwalimu. Alihamia timu ya Ligi ya Kuu ya Kenya ya Shabana Kisii. Mwaka wa 1998 alihamia timu ya AFC Leopards na walishinda taji la ligi mwaka huo. Kisha alihamia Mathare United na baadaye alihamia klabu za Al-Ismaily, Chuo Kikuu cha Park na kisha akapata fursa kwenda katika nchi ya Uswidi kuichezea klabu ya Skellefteå FF.

Mulama alianza kozi ya ukufunzi katika udhamini wa soka nchini Marekani akiwa katika Chuo Kikuu cha Missouri na mwaka wa 2008 alikuwa Mkufunzi mkuu wa klabu ya AC Nakuru.

Hata hivyo, alirejea uwanjani mwaka wa 2009 na aliichezea klabu yake ya zamani ya Mathare United.

Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Simeoni ni pacha wa mchezaji mwenzake Titus Mulama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Mchezaji Soka wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simeon Mulama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.