Shule ya Wavulana Tabora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shule ya Wavulana Tabora (maarufu kama Tabora boys au Tabora school) ni mojawapo ya shule kongwe nchini Tanzania.

Shule hii ilianzishwa mnamo mwaka 1922. Ilikuwa moja ya shule 3 za serikali ya kikoloni kwa ajili ya wavulana Waafrika, hasa kwa watoto wa machifu. Hadi miaka ya 1950 hivi ilikuwa shule ya pekee ya serikali kwa ajili ya Waafrika iliyoendelea hadi mwisho wa sillabasi ya sekondari yaani dara sa la 12. [1]

Leo ni miongoni mwa shule za watoto wenye vipaji maalumu

Shule ya Wavulana Tabora

.[2]

Miongoni mwa watu maarufu waliosoma katika shule hii ni Rashidi Kawawa, Kaluta Amri Abeid pamoja na baba wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.[3] Kupata orodha fupi angalia hapa

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Clarke, Philip. Notes on Pre-Independence Education in Tanganyika; Occasional Papers, 34, Southampton Univ. (England). Centre for Language Education.1995, uk. 17ff
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-07-12. Iliwekwa mnamo 2020-02-05.
  3. https://www.ippmedia.com/sw/makala/tabora-boys-1922-2016-shule-iliyozalisha-safu-nzima-ya-serikali
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shule ya Wavulana Tabora kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.