Shule ya Upili ya ELCK Kenyoro
Shule ya Upili ya ELCK Kenyoro ni shule ya mseto inayopatikana katika mtaa wa Kenyoro, Kata ya Itibo, Ekerenyo katika kaunti ya Nyamira, nchini Kenya.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Shulu ya E.L.C.K. Kenyoro ilianzishwa mnamo mwaka wa 1997 kwa msaada wa Kanisa la ELCK Kenyoro. Ilianza na wanafunzi wachache sana, ikiwa wengi wao ni wa kujitolea ili kuwashawishi wengine wajiunge nao. Haikuwa na walimu waliohitimu wa Serikali kwa wakati huo. Wanafunzi wa kwanza walifanya mtihani wa Kitaifa (K.C.S.E) mnamo mwaka wa 1999.
Hatimaye Shule hii ilitambuliwa rasmi na serikali mnamo 2000 kama chuo cha mafunzo cha serikali.
Ilitumiwa mwalimu mkuu wa kwanza aliyehitimu Bwana Charles Nyandoro Moochi mnamo 2001. Wakati huu, shule hii ilikuwa na wanafunzi takribani 180.
Mazingira
[hariri | hariri chanzo]Shule ya Upili ya ELCK Kenyoro iko mashinani mtaani Kenyoro. BArabara kuu iliyo karibu ni ile ya Nyamira-Ikonge iliyo takribani kilomita 3 kutoka Shuleni humo.
Inapakana na Shule ya msingi ya ELCK Kenyoro, Kanisa la ELCK Kenyoro na Hospitali Ndogo ya KEnyoro.Shule hii pia imepakana na maskani ya Mbunge wa Mugirango Kaskazini (2007-2012) Bwana Wilfred Ombui Kabete.
Ukosefu wa barabara bora katika eneo hili ni miongoni mwa vikwazo inaxyopambana navyo shule hii.
Michezo
[hariri | hariri chanzo]Ingawa ni shule ndogo,imewahi kujifunia umaarufu katika wilaya ya Nyamira hasa katika mchezo wa Handiboli katika miaka ya 2006,2007,2008 na 2009 chini ya ukufunzi wa Thomas Mogita. Isitoshe, shule hii inajulikana kwa umaarufu wake katika riadha, huku ikijifunia wanariadha wa Masafa marefu kama vile Clinton Mayaka, Evans Mayaka na Catherine Ombogo.
Matokeo ya Kielimu
[hariri | hariri chanzo]Shule hii imekuwa ikiendelea kukikuza kiwango cha elimu mwaka baada ya mwingine. Ilitoa wanafunzi waliofuzu kujiunga na Vyuo vikuu vya serikali kwa mara ya kwanza mnamo 2002 ambapo wanafunzi watatu, William Mose, Jackline Maosa (marehemu) na Metal Otiso walifuzu kuingia vyuo vikuu. Mnamo mwaka wa 2003, kulikuwa na mwanafunzi mmoja aliyefuzu, Justus Michira. Mnamo Mwaka wa 2004, Josephine Maosa ndiye aliyeipeperusha bendera ya Kenyoro, huku akifuzu na alama 72, ambayo ni alama ya juu zaidi kurekodiwa kufikia mwaka huo. Mnamo mwaka wa 2005, kulikuwa na mwanafunzi mmoja aliyafuzu pia, Joshua Nyaundi. Mwaka wa 2006 hakukuwa na mwanafunzi aliyefuzu, huku wanafunzi wawili, Daglas Nyangoka na Mary Bitoyo wakikosa kwa ufinyu kufuzu. Shule hii ilipata umaarufu wilayani mnamo mwaka wa 2007 wakati ilipata alama ya A kwa mara ya kwanza kupitia kwa mwanafunzi Samson Maosa ambaye alikuwa wa Pili katika wilaya mpya ya Nyamira. Wakati huo,kulikuwa na wanafunzi wawili tu waliopata alama ya A katika wilaya mpya ya Nyamira, mwingine akitoka katika Shule ya Upili ya Masosa.
Majengo
[hariri | hariri chanzo]Kufuatia ufinyu wa ardhi, shule hii imejenga madarasa 4 huku kila kidato kikiwa na chumba kimoja. Isitoshe kuna majengo mengine ya Ofisi za Walimu, Maabara na Maktaba.