Kanisa la ELCK Kenyoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lango la Kanisa ya Kenyoro.

Kanisa la ELCK Kenyoro ni mojawapo kati ya makanisa ya kwanza ya Walutheri nchini Kenya.

Anwani ya kijiografia[hariri | hariri chanzo]

Kanisa hili linapatikana katika mtaa wa Kenyoro, kata ya Itibo, divisheni ya Ekerenyo, Kaunti ya Nyamira, nchini Kenya.

Limepakana na Shule ya Upili ya ELCK Kenyoro na Hospitali Ndogo ya Kenyoro.

Makanisa mengine yaliyo karibu ni pamoja na Kanisa la ELCK Nyagokiani, Kanisa la ELCK Erandi, Kanisa la ELCK Ekerubo Gietai, Kanisa la ELCK Getangwa, Matunwa SDA, Kanisa la ELCK Matorora na Kanisa la ELCK Menyenya.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kanisa hili la Kilutheri lilikuwa la pili kuanzishwa katika Wilaya ya Nyamira na wamisionari wakati wa ukoloni baada ya Matongo.

Ujenzi wake uliisha mnamo 1986.

Makanisa ya Ushirika wa Kenyoro[hariri | hariri chanzo]

Kama makao makuu ya ushirika wa Kenyoro, kanisa la Kenyoro ni moja kati ya makanisa manne ya Ushirika huu. Mengine ni:

Idadi ya washiriki[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya washirika imezidi kuongezeka tangu kuanzishwa, jambo ambalo lilipelekea kugawanywa kwa kanisa hili kuunda makanisa mengine ambayo yaliunda Wilaya ya Ushirika ya Nyamira Borabu.

Sasa hivi kuna takriban washirika 600.

Majengo[hariri | hariri chanzo]

Kuna jengo kuu la ibada pamoja na jengo jingine dogo linalotumiwa kama makao ya mhubiri.

Jengo la tatu linatumika kama ofisi kuu ya Wilaya ya Ushirika ya Nyamira Borabu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]