Shule ya St Andrews, Turi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shule ya St. Andrews ni shule huru ya msingi na ya sekondari mjini Nakuru, Kenya, karibu na mji wa Molo. Inajulikana kwa jina la "Turi" ambalo ni jina la kijiji kilicho karibu na hapo.

Shule hii ni ya Kikristo, ambapo wanafunzi hulala kwenye mabweni. Inatumia mfumo wa elimu wa Kiingereza kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 5-13 katika shule ya msingi, na miaka 13-16 katika Shule ya Upili. Shule hii imejengwa kwenye uwanja wa ekari 300, katika miinuko ya Kenya, mjini Turi.

Shule hii ina wanafunzi wa kutoka Kenya na nchi jirani za Afrika Mashariki, na pia ina idadi ya wanafunzi wanaotoka nchi za nje, wengi wakiwa watoto wa walioleta dini ya Kikristo wa Kiprotestanti. Kwa vile mfumo wa elimu ni wa Kiingereza, walimu wengi wa wamepata mafunzo ya mfumo huu wa Kiingereza, na wanafunzi wengi ni wa kutoka familia za Kiingereza wanaoishi nchini Kenya. Wanaporejea nchini Uingereza, wanafunzi wengi hujiunga na shule za kibinafsi kama Shule ya Stowe, mjini Buckingham, Shule ya Dean Close mjini Cheltenham au Shule ya Monkton Combe mjini Bath. Wafanyakazi wengi mwishowe huenda kufundisha katika shule ya Monkton Combe, mjini Bath, mwelekeo ambao utaendelea katika siku zijazo.

Mwalimu mkuu wa shule ya upili hivi sasa ni Adrian Palmer na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ni Paddy Moss.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Shule ya msingi ilianzishwa mwaka wa 1931 na Bw na Bi Lavers, waliojulikana kama "Ma na Pa Lavers", ili kusome. Shule ya kwanza ilikuwa na watoto 15 lakini iliimarika na kuhudumu zaidi ya watoto 100 mnamo mwaka wa 1940 kutoka nchi za Kenya na Uganda. Mwaka wa 1944, shule yote ilichomeka na kuteketea baada ya moto ulioanza jikoni. Serikali ya kikoloni ya Uingereza ilitoa ruhusa kwa wafungwa wa vita wa Kiitaliano kusaidia kujenga shule mpya kwa sababu gharama ya kujenga tena jumba upya ilikadiriwa kuwa ghali sana. Nembo ya shule huonyesha ndege wa moto anayefufuka kutoka kwa moto, na kila mara moja kwa mwaka moto huwashwa ili kupata kumbukumbu ya kipindi hiki katika historia ya shule. Shule hii ilimalizika kujengwa wakati wa miaka ya 1950 wakati Lavers walikuwa katika umri wao wa kati na majengo mapya yakamalizwa. Mwaka wa 1988 shule ya sekondari ilifunguliwa kwa watoto wa umri wa miaka 13-16.

Shule ya Msingi[hariri | hariri chanzo]

Wanafunzi hufundishwa ndani ya darasa kuanzia umri wa miaka mitano. Baada ya hapo, masomo tofauti tofauti huanza kufundishwa mpaka maeneo yote ya masomo yamefundishwa na walimu wataalamu katika Darasa ya 6 na 7. Wanafunzi wakifika darasa la 8, wanafunzi wako tayari kufanya mtihani wa IAPS ambayo hujumuisha masomo saba (Kiingereza, Hesabu, Sayansi, Kifaransa, Jiografia, Historia na Masomo ya Kidini).

Shule ya Upili[hariri | hariri chanzo]

Masomo mengi hufunzwa kwenye Darasa la 9, inayohakikisha uchaguzi bora wa masomo ya IGCSE katika Darasa la 10 na 11. Baada ya kumaliza IGCSE, wanafunzi hufuata mfumo wa AS/A2 au IB diploma. Wengi wao huendelea kusoma katika nchi za Afrika Mashariki, Uingereza, Afrika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini, wengi wao wakipata misaada ya kusomea masomo kama vile katika muziki au michezo, na mengineyo.

Taasisi ya Mafunzo[hariri | hariri chanzo]

Shule hii itaimarisha elimu ya wanafunzi wake kwa kuchukua hatua ya kuendeleza masomo ya wanafunzi wa kidato cha Sita hivi karibuni. Ina mipango ya kufungua milango yake mnamo Septemba 2010, kwa kufundisha wanafunzi wa kidato cha sita masomo ya 'A' Level ili kusaidia wanafunzi kuanza kujiandaa kwa maisha ya chuo kikuu.

Michezo ya ziada[hariri | hariri chanzo]

Michezo ni sehemu muhimu ya maisha ya wanafunzi wa shule ya St Andrew's. Vifaa kwenye uwanja wa ekari 300 ni kama bwawa la kuogelea lamaji ya moto, vyumba vya kecheza tenisi, na uwanja mkubwa wa kucheza michezo mengineyo ambayo hukaa rangi ya kijani mwaka mzima. Pia, wana mpango wa kujenga ukumbi mpya wa michezo katika hivi karibuni.

Wanafunzi wanahimizwa kuendeleza vipaji vyao vya kibinafsi kwa kupitia sanaa, muziki na maigizo.

Malezi[hariri | hariri chanzo]

Wanafunzi wengi hulala kwenye bweni muda wote, na wachache hulala kwenye bweni siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Timu za malzi huchungaji ustawi wa kila mtoto.

Wanafunzi maarufu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]