Nenda kwa yaliyomo

Shenazi Salum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Shenazi)
Shenazi Salum
Shenazi akiwa katika pozi
Shenazi akiwa katika pozi
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Nchi Mtanzania
Alizaliwa 1972
Alikufa 8 Septemba 2007
Aina ya muziki Uimbaji
Kazi yake Mwigizaji filamu na mwimbaji
Miaka ya kazi mn. 1992 hadi 2007
Ameshirikiana na Mwajuma Thabiti
Ala sauti

Shenazi Salum (1972 - 8 Septemba 2007 ) alikuwa muigizaji, mchezaji wa muziki wa kujitegemea na pia kungwi yaani mtu anayefundisha waakina mama namna ya kukaa na mume (Kitchen Paty).

Shenazi alizaliwa jijini Dar es Salaam, Tanzania na kufariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Tunduma karibu kidogo na mji wa Mbeya, Tanzania.

Kwa mara ya mwisho alishiriki katika filamu ya "Kitchen Party" akiwa kama kungwi pamoja na rafiki yake wa karibu aiitwaye "Mwajuma Thabiti" maarufu kama "Rose Jimama". Ni filamu yenye kuonyesha namna ya kuishi vizuri na mume na mambo mengine mengi tu yenye faida kwa walengwa hususani akina mama. Malkia wa kunengua miondoko ya Taarab na Mduara nchini, Shenazi Salum pichani ni miongoni mwa watu 27, waliokufa kwenye ajali ya basi, iliyotokea juzi kwenye Kijiji cha Majenje, Mbarali, Mbeya.

Kwa mujibu wa mdogo wa mwanamuziki huyo aitwaye Hanifa Salum, Shenazi alifariki dunia, muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo, iliyohusisha magari matatu....

alisema, Shenazi alipata ajali hiyo, alipokuwa akirejea nyumbani kwake Dar es Salaam na alikuwa akitoka Tunduma, Mbeya kwenye shughuli zake za muziki “Alituaga kwamba anakwenda Mbeya kufanya ‘shoo’, hatukujua kama ndiyo kifo kilikuwa kinamwita, lakini ndiyo hivyo Mungu kamchukua,” alisema Hanifa huku akitokwa na machozi.

Rafiki wa Shenazi ambaye naye ni mnenguaji maarufu, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama’, anasema kuwa marehemu alikwenda Mbeya na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Tuki.

Rose alisema: “Nilipata taarifa kama Shenazi amepata ajali, nikapiga namba yake, ikapokelewa na polisi mmoja huko Mbeya, nikamuomba nataka kuongea na Shenazi, akanijibu, unataka kuongea na maiti? “Nilichanganyikiwa, yule polisi aliniambia rafiki yangu Shenazi amekufa na Tuki hali yake ni mbaya, nidhani utani, lakini yote ni mipango ya Mungu.”

Habari zaidi zilisema kuwa rafiki huyo wa Shenazi, Tuki, amevunjika miguu yote na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala, Mbarali. Shenazi alikuwa kwenye basi la SABCO aina ya Scania, T443 APF ambalo liligongana na lori pamoja na magari mawili yanayomilikiwa na Halmashauri ya Mbarali.

Ajali hiyo iliyoua watu 27, ilisababisha majeruhi 33. Shenazi alitarajiwa kuzikwa jana ambapo mwandishi wetu walifika nyumbani kwao, Ilala, Dar es Salaam na kukuta taratibu za mazishi zikiwa zimeshaanza kufanywa. Mbali na kunengua, malkia huyo atakumbukwa kama kungwi, aliyekuwa akiwafunda watu kabla ya ndoa, pia ni mwigizaji ambapo enzi za uhai wake aliwahi kucheza Filamu ya Kitchen Party ambayo ilipata umaarufu mkubwa.]]

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shenazi Salum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.