Nenda kwa yaliyomo

Shams al-Baroudi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shams al-Muluk Gamil al-Baroudi

Amezaliwa Misri
Kazi yake Mwigizaji wa Filamu
Ndoa aliolewa na Hassan Youssef

Shams al-Muluk Gamil al-Baroudi (Kiarabu: شمس الملوك جميل البارودي‎) ni mwigizaji mstaafu Egyptian ambaye alikuwa akifanya kazi katika Egyptian films na pia Lebanese Films kuanzia mwaka 1960 hadi 1970. Lisa Anderson wa Chicago Tribune alimtaja kama “Mmoja wa waigizaji warembo na wakuvutia Zaidi wa Misri”.

Alizaliwa kwa baba na mama wa Misri, al-Baroudi alisoma katika Taasis ya Juu ya Sanaa ya Tamthilia huko Cairo kwa miaka miwili na nus una akaigiza kwa mara ya kwanza katika sinema ya vichekesho vya Ismai Yassin ‘’Hiredd Husband’’ ( زوج بالإيجار) Mnamo 1969. Baada ya kazi nzuri katika miaka ya 1960, Alianza kuangaziwana majukumu ya “transgressive” mapema miaka ya 1970.

Baada ya ndoa na mwigizaji mwenza Hassan Youssef mwaka wa 1972, wanandoa hao walianza kufanya kazi kwa ushirikiano hadi al-Baroudi alipoamua baada ya Umrah mwaka wa 1982, kuacha sinema na kuvaa hijabu. Wakati huo Youssef alikuwa bado anarekodi filamu ya Two on the Road (اثنين على الطريق) na baada ya al-Baroudi kustaafu bila kutarajiwa, filamu hiyo iliweza kukamilika na kutolewa tu kufikia 1984.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shams al-Baroudi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.