Shaaban Idd Chilunda
Shaaban Idd Chilunda (alizaliwa Tandahimba, 20 Juni 1998) ni mchezaji wa soka wa timu ya taifa ya Tanzania ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu iliyopo nchini Tanzania ya Azam.
Kazi ya klabu
[hariri | hariri chanzo]Chilunda alijiunga na klabu ya vijana ya Azam FC mwaka 2012. Alicheza kwa mara yake ya kwanza mwaka 2016, na tarehe 9 Julai 2018, alifunga magoli manne katika ushindi wa nyumbani wa 4-2 dhidi ya Rayon Sports FC katika mashindano ya Kagame Interclub Cup, pia alifunga goli moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba SC.
Tarehe 7 Agosti 2018, Chilunda alikubaliana na mpango wa mkopo wa miaka miwili upande wa Hispania katika ligi ya Segunda División akiwa na klabu ya CD Tenerife, baada ya kipindi cha majaribio. Alicheza mechi yake ya kwanza kwa siku kumi na tatu baadaye, akiingia kama mbadala wa mchezaji ambaye ni marehemu Filip Malbašić katika mechi waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Gimnàstic de Tarragona.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shaaban Idd Chilunda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |