Nenda kwa yaliyomo

Severino Poletto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Severino Poletto

everino Poletto (18 Machi 193317 Desemba 2022) alikuwa kardinali wa Italia katika Kanisa Katoliki ambaye alihudumu kama Askofu Mkuu wa Turin kuanzia 1999 hadi 2010. Alikuwa askofu tangu mwaka 1980 na alipewa hadhi ya kardinali na Papa John Paul II mwaka 2001.

Poletto alizaliwa Salgareda, Veneto, tarehe 18 Machi 1933, akiwa mtoto wa mwisho kati ya watoto 11, ambapo 9 walinusurika utotoni. Familia yake ilihamia Piedmont mwaka 1952 kutafuta kazi. Alisoma katika seminari ya Treviso na kisha katika seminari kuu ya Casale Monferrato, mkoani Alessandria. Alipadrishwa tarehe 29 Juni 1957 na Askofu Giuseppe Angrisani wa Casale Monferrato. [1]

  1. Acts Apostolicae Sedis (PDF). Juz. la LXXII. 1980. uk. 330. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.