Sethembile Msezane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Sethembile Msezane
Faili:Ethembile Msezane- Portrait.jpg
Msanii Sethembile Msezane
Amezaliwa1991
KwaZulu-Natal
Kazi yakemsanii, mshereheshaji na muongeaji wa Afrika ya Kusini


Sethembile Msezane (amezaliwa KwaZulu-Natal, ) ni msanii, mshereheshaji na muongeaji wa Afrika ya Kusini anayetambulika zaidi kutokana na kazi za sanaa.

Msezane anatumia ujuzi wake katika fani mbalimbali zinazojumuisha upigaji picha, filamu, uchongaji sanamu na uchoraji kuweka bayana masuala ya kidini, kisiasa na ujuzi wa Kiafrika. Kazi za Msezane zipo katika makumbusho ya Afrika Kusini pamoja na dunia nzima na ameshinda tuzo nyingi.[1]

Msezane ni mwanachama wa ‘’iQhiya Collective’’, mtandao wa wanawake Weusi ambao ni wasanii kutoka Cape Town, Johannesburg na kwingineko Afrika Kusini.

Sethembile Msezane, Signal Her Return III, 2019. Akiwa na Tyburn Gallery.

Elimu na kazi[hariri | hariri chanzo]

Japokuwa ni mzawa wa Kawazulu-Natal, Msezane alikulia Johannesburg. Baadaye alihamia Cape Town, ambako alijiunga na chuo kikuu cha ‘’Michaelis School of Fine Art’’ kusoma shahada ya sanaa mwaka 2012 kisa shahada ya uzamili mwaka 2017.[1][2] Maonyesho ya Msezane yanalenga ukosekanaji wa wanawake katika siasa na mandhari ya historia nchini Afrika Kusini. Kupitia maonyesho yake, anaelezea ni kwa namna gani wanawake wamekua wakizuiwa na jamii katika jitihada zao, mavazi na kufanya utambuzi kwa kutumia mwili wake kama sanamu kwa kuvaa kama kiashiria kwenye mavazi kukazia umuhimu wwake, uwepo na uhusika katika sehemu za wazi.[3]

Kazi za Msezane zimetambulika kwa kiasi kikubwa ulimwenguni kwote na katika makumbusho ya Afrika Kusini ikiwemo ‘’Iziko South African National Gallery’’, ‘’Zeitz Museum of Contemporary Art Africa’’ na ‘’University of South Africa’’.[1] Mwaka 2016 Msezane alikua mtu wa kwanza kupata tuzo ya ‘’Rising Light Award’’ wakati wa tuzo za Mboko. Alipata pia tuzo za TAF na SYLT Emerging Artist Residency (TASA) mwaka huohuo na alifika kumi bora mashindano ya Barclays L'atelier. Msezane aliteuliwa pia katika tuzo za ‘’ANTI – Contemporary Art Festival’’ mwaka 2017.[4]

Kazi yake, "Chapungu-the Day Rhodes Fell" (2015) ilionyeshwa wakati wa maandamano ya ‘’Rhodes Must’’, wakati huo sanamu ya John Cecil Rhode iliyopo Chuo kikuu cha Cape Town ilikua ikiodolewa. Msezane alisimama kama sanamu mtu kwa muda wa masaa katika maonyesho ya kutaka kuchukua nafasi ya sanamu ya Rhodes. Msezane amekua akitumia siku za mapumziko nchini Afrika Kusini kutumbuiza na kuelezea juu ya masuala yanayo athiri vijana wa sasa, hii ilikua ni kama sehemu ya maonyesho yake ya "Public Holiday 2014-2015" [3] Maonyesho mengine ya Msezane inajumuisha "Kwasuka Zukela" (2017) Maonyesho ya MoMo, Cape Town, Afrika Kusini, "All Thing being Equal" Zeitz Mocca (2017)Cape Town, Afrika Kusini na "Unframed"(2018) katika maonyesho ya sanaa ya Cape Town. Msezane alifanya maonyesho yake ya kwanza nchini Uingereza "Speaking through the wall" katika makumbusho ya Tyburn Gallery, London (2019), pamoja na kazi yake mpya ya "Signal her return III" huko Nottingham, Uingereza.[1]

Msezane pia amefanya maonyesho ya vikundi baadhi zikiwa kama "Women's Work and the art of Disruptions"(2016) huko Iziko Afrika Kusini, "Re-assisting narratives’’(2016) Amsterdam, "Dancing on a Volcano"(2018) Nigeria, "Translations" (2015) Portland, Oregon, "Made Visible: Contemporary South African Fashion and Identity" (2019), Boston, Marekani.[5][1]

Msezane alikua kama muongeaji kwenye TedGobal mwaka 2017.[5]Y

Maonyesho[hariri | hariri chanzo]

"Speaking Through the Wall" (2019) Tyburn. London, Uingereza[1]

"Kwasuka Sukela" (2017) Momo. Cape Town, Afrika Kusini[1]

"All Things Being Equal" (2017) Zeitz Mocca. Cape Town, Afrika Kusini[1]

"Unframed" (2018) Cape Town Art Fair. Cape Town, Afrika Kusini.

"Umoya: a Quiet revolution" maonyesho ya sanaa ya FNB Joburg. Johannesburg, Afrika Kusini[1]

"Re(as)sisting Narratives" (2016) Framer Framed, Amsterdam, Uholanzi

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • OkayAfrica|Okay Africa 100 Women 2018 mshindi[4]
  • Mbokodo Award mtu wa kwanza kupata tuzo ya Light Award 2016[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 Sethembile Msezane (en-GB).
  2. "Sethembile Msezane - Zeitz MOCAA", Zeitz MOCAA. (en-US) 
  3. 3.0 3.1 "5 young artists who have us excited about politics | Live Mag", Live Mag, 2015-10-02. (en-US) 
  4. 4.0 4.1 "Sethembile Msezane", OKAYAFRICA's 100 WOMEN. Retrieved on 2021-04-10. (en-US) Archived from the original on 2021-04-10. 
  5. 5.0 5.1 Msezane, Sethembile. Sethembile Msezane | Speaker | TED (en).
  6. Msezane, Sethembile. "Sethembile Msezane | Speaker | TED". (en) 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sethembile Msezane kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.