Serge Gnabry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gnabry akikimbiza mpira.

Serge David Gnabry (alizaliwa 14 Julai 1995) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Ujerumani ambaye anacheza kama winga wa klabu ya Bundesliga Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani.

Gnabry alianza kazi yake huko Uingereza na klabu ya Arsenal. Alikwenda kwa mkopo West Bromwich Albion na baadae alirudi nyumbani Ujerumani kujiunga na Werder Bremen 2016.

Mnamo mwaka 2017 alisaini Bayern Munich, Katika msimu wake wa kwanza na Bayern Munich alitwaa taji la Bundesliga na alipewa mchezaji bora wa msimu, Mnamo 1 Oktoba 2019, Gnabry alifunga mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika ushindi wa 7-2 dhidi ya Tottenham Hotspur.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Serge Gnabry kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.