Semih Kaplanoğlu
Mandhari
Semih Kaplanoğlu (alizaliwa 4 Aprili 1963) ni mwandishi, mkurugenzi na mtayarishaji wa filamu kutoka Uturuki.[1]
Maisha na kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1984, Semih Kaplanoğlu alihamia Istanbul na kufanya kazi kwa miaka michache kama mwandishi wa matangazo katika kampuni kama Güzel Sanatlar Saatchi & Saatchi na Young & Rubicam.
Mwaka 1986, alihamia kwenye tasnia ya sinema, akawa msaidizi wa mpiga kamera kwa filamu mbili za makala za kihistoria zilizoshinda tuzo.
Mnamo mwaka 1994, Kaplanoğlu aliandika na kuongoza mfululizo wa televisheni Şehnaz Tango, uliojumuisha vipindi 52 na kurushwa hewani kwenye vituo vya Show TV na InterStar, na ukafanikiwa sana.[2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Semih Kaplanoğlu Retrieved 2019-11-07.
- ↑ "Bala Altın Ayı", 2010-02-20. Retrieved on 2019-11-07. (tr)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Semih Kaplanoğlu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |