Sementi ya meno
Mandhari
Sementi ya jino (kutoka Kilatini cementum) ni dutu inayofanana na aina ya mfupa na kufunika uso wa dentini ya kizizi cha jino. Ni ganda jembamba linalotunza dentini na kuishika katika ufizi wa meno na kitundu cha taya.
Sementi hii inafanywa hasa kwa kampaundi ya kalisi inayoitwa apatiti hidroksili (Ca5[OH|(PO4)3]). Kama kampaundi zote za kalisi inaweza kuyeyushwa kwa asidi na hivi uchafu mdomoni unaoruhusu kustawi kwa bakteria zinazotengeneza asidi ni hatari kwa afya ya meno.
Ndiyo sababu ya umuhimu wa kupiga mswaki na kusafisha meno mara kwa mara, hasa kwa watu wanaotumia sukari katika chakula na vinywaji.
Sementi hii inaendelea kujengwa upya na seli za pekee.
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sementi ya meno kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |