Schweppes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Schweppes[hariri | hariri chanzo]

Schweppes.com

Bonyeza picha hii kuingia tovuti kamili ya Schweppes

Historia[hariri | hariri chanzo]

Schweppes ni kinywaji kinachoundwa na kuuzwa kote duniani. Inahusu aina mbalimbali kama ya maji yenye kabondayoksaidi na sharubati yenye tangawizi. Kampeni ya mauzo ilitumia sana sauti ya "Schhhh .......Schweppes" katika kurekodi kwa televisheni ili kuiga sauti ya gesi inapotoka chupa inapofunguliwa.

Mwishoni mwa karne ya kumi na nane, Johann Yakobo Schweppe(1740-1821), aliyekuwa amezaliwa Ujerumani lakini akawa muundaji wa saa na mwanasayansi huko Uswidi,alivumbua mchakato wa kutengeneza maji yenye kabondayoksaidi.Alianzisha Kampuni ya Schweppes katika jiji la Geneva(1783). Katika mwaka wa 1792 alihamia jiji la London ili kuendeleza biashara huko.

Bidhaa[hariri | hariri chanzo]

Bidhaa za msingi alizounda ni sharubati ya tangawizi(1870),sharubati ya machungwa machungu(1957) na maji ya toniki(kinywaji laini chenye ni kongwe kabisa duniani - 1771) Kampeni ya Schweppes,katika filamu ya runinga, ya miaka kati ya 1950 na 1960 ilionyesha mwanajeshi mkongwe wa vita wa Uingereza aliyeitwa Kamanda Whitehead akinywa kinywaji cha Schweppes na kuita hisia ya kukinywa kinywaji hicho kama "Schweppervescence".Alielezea kuwa hii ndio ile utamu mtu anapohisi akinywa kinywaji kilichotiwa na kuchanganywa na kabondayoksaidi.Baada ya hii Kamanda Edward Whitehead alijulikana zaidi kama mwakilishi wa kinywaji cha Schweppes.Aliendelea na akawa Rais wa Schweppes(USA) na Meneja Mkuu(Kampuni za Ng'ambo)

Mojawapo ya bidhaa za Schweppes-Sharubati ya machungwa machungu

Katika nchi ya USA,bidhaa za Schweppes zinaundwa viwandani na Kundi la Dr Pepper Snapple Katika nchi nyingine ikiwemo Uingereza, Brazili, Bulgaria na Uturuki,bidhaa hizo huundwa viwandani na kampuni ya Coca Cola Katika Ujerumani na Austria,bidhaa zote za Schweppes zinaundwa viwandani na kampuni ya Krombacher Brauerei chini ya kibali cha kampuni ya Schweppes. Schweppes ya Ujerumani(iko pamoja na Krombacher)wote hudhibiti leseni za Kijerumani na Austria kwa kampuni ya Snapple (kampuni hii haipatikani katika Ujerumani au Austria),kampuni ya Dr Pepper na Orangina. Mnamo wa mwaka wa 2009,kampuni ya [Cadbury] iliuzia Asahi Breweries sehemu yake ya biashara katika kampuni ya Schweppes ya Australia na kuifanya soko ya mwisho ambayo Cadbury iliachana na kampuni hiyo.

Kampuni ya Schweppes wameendelea na uzinduzi wa aina mbalimbali ya vinywaji na kupata soko kubwa kote duniani. Schweppes ilikuwa mdhamini katika mipango mbalimbali kama 2008 Schweppes Concours D'Elegance ambayo ni mashindano ya magari ya kitambo ili kuona gani ni bora zaidi.

Vinywaji mbalimbali kutoka kampuni ya Schweppes

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kamanda Whitehead

Krombacher

Vinywaji visivyolevya watu

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: