Santha Rama Rau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Santha Rama Rau
शान्ता राम राव
Amezaliwa 24 Januari 1923
India
Amekufa 21 Aprili 2009
New York, Marekani
Kazi yake Mwandishi
Ndoa Faubion Bowers (1951-1966)
Gurdon Wattles (1970-1995)

Historia[hariri | hariri chanzo]

Santha Rama Rau (शान्ता राम राव) (24 Januari 1923 - 21 Aprili 2009) alikuwa mwandishi wa kusafiri.

Baba yake, Sir Benegal Rama Rau, alikuwa mwanadiplomasia na balozi wa Uhindi. Mama yake alikuwa Dhanvanthi Rama Rau, kiongozi katika harakati za kupigania haki za wanawake. Alikuwa pia Rais wa Muungano ya Kimataifa ya Kupanga Uzazi.

Chuo cha Wellesley( alichosomea Santha )kilivyo sasa huko Wellesley, Massachusetts

Hapo awali[hariri | hariri chanzo]

Kama kijana, Rama Rau aliishi katika Uhindi chini ya utawala wa Uingereza. Wakati yeye alikuwa umri wa miaka sita,aliandamana na baba yake katika ziara ya kisiasa ya Uingereza. Akiwa huko alipata elimu yake katika Shule ya Wasichana ya Mtakatifu Paulo na akamaliza katika mwaka wa 1939. Baada ya muda mfupi wa kusafiri kwa njia ya Afrika ya Kusini, yeye alirudi Uhindi kugundua mahali huko kulikuwa tofauti na yeye alivyokumbuka. Akaomba nafasi katika Chuo cha Wellessley, Wellessley,Massachusetts nchini Marekani na alikuwa mwanafunzi wa kwanza huko kutoka Uhindi. She alifuzu kwa kupita sana katika mwaka wa 1944. Muda mfupi baadaye, yeye alchapisha kitabu chake cha kwanza Home to India.

Uhindi ulipopata uhuru wake kutoka wakoloni katika mwaka wa 1947, baba yake Rama Rau aliteuliwa kama balozi wa kwanza wa Uhindi nchini Ujapani. Alipokuwa Tokyo, Ujapani, alikutana na mume wake wa baadaye,Mwamerika , Faubion Bowers. Baada ya kusafiri sana kote Asia na kidogo Afrika na Uropa, Rama Rau na Bowers waliishi jijini New York.Rama Rau akawa ni mwalimu katika Idara ya Kiingereza ya Chuo cha Sarah Lawrence,Bronxville ,New York katika mwaka wa 1971 ,akifanya kazi pia kama mwandishi.

Maktaba ya Chuo cha Sarah Lawrence,ambako Santha alifanya kazi katika Idara ya Kiingereza

Maisha ya baadaye[hariri | hariri chanzo]

Aliunda mchezo wa kuigiza kutoka riwaya A Passage to India kwa ruhusa ya mwandishi E.M. Forster. Mchezo huo ulitayarishwa na Oxford Playhouse ,Oxford,Uingereza na ukazuru hadi West End jijini London na kuigizwa mara 261 kisha ukazuru Broadway jijini New York na kuigizwa mara 109 tangu Januari 1962. Ilichukuliwa na John Maynard na kuelekezwa na Waris Hussein kama kipindi cha runinga katika stesheni ya BBC katika mwaka wa 1965. Katika mwaka wa 1984,mchezo huo ulichukuliwa na kutumika kuunda filamu na direkta David Lean.

Hadithi fupi yake, By Any Other Name, ni moja ya insha katika Gifts of Passage. Ipo katika Norton Anthology of English Literature na inatumika sana katika masomo.

Maisha ya binafsi[hariri | hariri chanzo]

Aliolewa na Faubion Bowers(1951) na akapata mwana mmmoja, Jai Peter Bowers katika mwaka wa 1952. Akapewa talaka katika mwaka wa 1966. Katika mwaka wa 1970, Rama Rau alifunga ndoa na Gurdon B, hakujifungua watoto. Faubion Bowers alikufa mwezi wa Novemba 1999 na anakumbukwa kwa kupitia mwana wake,Jai. Jai sasa anaishi Scottsdale, Arizona, pamoja na mke wake, Deborah Lee Bowers, na ana binti, Whitney Elizabeth Bowers. Jai pia ina wana wengine wawili, Morgan na Ross Mandeville.

Rau aliandika kitabu cha makumbusho fupi kilichoitwa By Any Other Name, kama ilivyotajwa hapo juu. "Yeye, akiwa umri wa miaka 5 na nusu na dada yake wa umri wa miaka 8,Premila, walienda shule ya Anglo-India ambako mwalimu aliwabadilisha jina ili yawe ya kiangliki. Jina lake Santha lilibadilishwa liwe Cynthia huku la Premila likiwa Pamela. Mazingira hayo waliyoishi na kucheza hayakuwa bora kwao. Walipokabiliwa na aibu ya mwalimu kusema kuwa "Wahindi hudanganya kwa mitihani", Premila alimchukua dada yake na wakatembea hadi nyumbani na hawakurudi shule hiyo tena."

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vilivyoandikwa na Rau ni:

 • Home to India
 • East of Home
 • This is India
 • Remember the House(Riwaya)
 • My Russian Journey
 • Gifts of Passage
 • The Adventures (riwaya)
 • View to the Southeast
 • A Princess Remembers
 • An Inheritance.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Weber, Bruce (24 Aprili 2009). "Santha Rama Rau, Who Wrote of India’s Landscape and Psyche, Dies at 86". The New York Times. http://www.nytimes.com/2009/04/24/arts/24ramarau.html.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

 1. Santha Rama Rau
 2. Orodha ya Vitabu vya Santha Rama Rau
 3. Santha Rama Rau
 4. By Any Other Name
 5. Santha Rama Rau