Sala ya chakula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sala ya chakula ni sala ambayo watu wa dini mbalimbali wanaomba baraka kwa vyakula vyao na baadaye wanamshukuru Mungu kwa kuwajalia.

Mfano ufuatao ndio uliozoeleka zaidi kati ya Wakatoliki wanaotumia lugha ya Kiswahili: Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina. Tubarikie Mungu wetu, sisi na chakula chetu tupate nguvu za kukutumikia vema. Amina. Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.