SMAUJATA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

SMAUJATA ni kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto nchini Tanzania iliyoanzishwa na Sospeter Mosewe Bulugu mwaka 2022 chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu[1]. Kampeni hulenga kupinga kila aina ya ukatili, ukiwemo ukatili dhidi ya watoto.

Smaujata inafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na taasisi za serikali zinazohusika katika kutoa haki, ambazo ni ofisi za Ustawi wa Jamii, polisi pamoja na Takukuru, hasa upande wa rushwa ya ngono.

Smaujata inafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na taasisi za serikali zinazohusika katika kutoa haki, ambazo ni ofisi za Ustawi wa Jamii, polisi pamoja na Takukuru, hasa upande wa rushwa ya ngono.

Malengo ya kampeni hiyo ni yafuatayo:

1. Kutambua na kutengeneza mtandao wa jamii wenye uwezo wa kupaza sauti kupinga, kupambana na kutokomeza ukatili dhidi ya Jinsia Zote Wanaume, wanawake, watoto na wazee.

2. Kuelimisha na kurahisisha utambuzi na ufanyiwaji kazi wa viashiria vyote vya ukatilii kuanzia ngazi ya familia.

3. Kuwatambua na kuwapongeza Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii waliofanikiwa kujitolea kushiriki kwenye Kampeni hii ili kuhamasisha wengine.

4. Kufikisha jumbe mbalimbali za wizara na serikali kwa ujumla kwenye jamii kupitia njia za utoaji elimu, ushirikishwaji wa wananchi kupitia makongamano.

Mfumo wa uratibu; Kutakuwa na timu za SMAUJATA kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kijiji na zitafanya kazi kwa karibu na maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii ngazi husika kupitia kiongozi wa timu ya SMAUJATA wa eneo husika ambaye atapewa barua ya utambulisho.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]