Nenda kwa yaliyomo

Robert Pattinson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robert Pattinson
Robert Pattinson

Robert Douglas Thomas Pattinson (amezaliwa Mei 13, 1986) ni muigizaji, mwanamitindo, mtayarishaji na mwanamuziki wa Uingereza.

Anajulikana sana kwa kucheza kama vampiri Edward Cullen kwenye sinema Twilight, na Cedric Diggory katika Harry Potter na Goblet of Fire.

Pattinson alizaliwa London, England. Akiwa na umri wa miaka kumi na mbili alifukuzwa shule. Baba yake alimuandikisha katika kilabu cha maigizo, na Pattinson alikiri kwamba alijiunga na kilabu kwa sababu ilikuwa nafasi ya kukutana na wasichana.

Amefanya kazi pamoja na Taylor Lautner, Kristen Stewart, Nikki Reed, Kellan Lutz, Jacson Rathbon na watu wengine wengi wakati akiigiza katika Twilight Saga. Ameshiriki katika sinema nyingi, kama vile The Haunted Airman, Remember Me, Little Ashes, Twilight, New Moon, Eclipse, n.k.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert Pattinson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.