Nenda kwa yaliyomo

Renato Corti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Renato Corti

Renato Corti (1 Machi 193612 Mei 2020) alikuwa kardinali na askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Italia.

Alikuwa Askofu wa Novara kuanzia mwaka 1990 hadi 2011. Papa Francis alimteua kuwa kardinali tarehe 19 Novemba 2016.

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Renato Corti alizaliwa Galbiate katika jimbo la Lecco, sehemu ya Jimbo Kuu la Milano, tarehe 1 Machi 1936. Alisoma katika seminari ya Milano na alipewa daraja la ukuhani tarehe 28 Julai 1959 na Kardinali Giovanni Battista Montini (baadaye Papa Paul VI). Majukumu yake yalijumuisha kuhudumu kama msaidizi wa paroko katika Oratory ya Caronno Pertusella kuanzia mwaka 1959 hadi 1967, mkurugenzi wa kiroho katika Chuo cha Gorla Minore kuanzia mwaka 1967 hadi 1969, na mkurugenzi wa kiroho wa seminari ya jimbo la Saronno kuanzia mwaka 1969 hadi 1977. Baadaye alikua mkuu wa masomo katika seminari ya Saronno na alikua na nafasi ya vicar mkuu wa Jimbo la Milan mnamo Novemba 1980.[1]

  1. "Italian Cardinal Corti, popular spiritual guide, dies at 84". Crux. 12 Mei 2020. Iliwekwa mnamo 13 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.