Rakuni
| Rakuni | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Rakuni wa Kawaida (Procyon lotor) | ||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||||||
|
Spishi 3: |
Rakuni (Kiingereza: Raccoon, kutahajiwa kama 'racoon' pia), mara nyingine anaitwa rakuni wa Amerika ya Kaskazini, rakuni wa kaskazini, au rakuni wa kawaida ili kumpambanua na spishi nyingine za rakuni, ni mamalia wa asili ya Amerika ya Kaskazini. Rakuni ni mnyama mkubwa zaidi wa familia ya jeni procyonid. Ana urefu wa mwili kati ya sentimita 40 na 70 (kati ya inchi 16 na 28), na uzito wa mwili kati ya kilo 5 na 26 (kati ya ratili 11 na 57). Wanaume huwa wakubwa zaidi kuliko wanawake. Manyoya ya kijivu yake ni manene, ambayo yanamlinda dhidi ya hali ya hewa baridi. Sehemu za kutofautisha zaidi za sura yake ni wayo wake ambao ni wepesi sana, kinyago chake, na mkia wake wenye pete. Sura hizi ni mada za visasili vya watu wa asili wa Amerika. Rakuni ni maarufu kwa sababu ya akili yake; mitaala yanaonyesha kwamba rakuni wanaweza kukumbuka majibu ya kazi ambazo anapwa baada ya miaka mitatu. Kwa kawaida rakuni huwa hai usiku, na hula chochote; asilimia 40 ya chakula chake ni wanyama wasio na uti wa mgongo, asimilia 33 ni mimea, na asimilia 27 ni wanyama wenye uti wa mgongo.
Makazi ya asili ya rakuni ni misitu ya kupukutika majani yake na misitu ya mchanganyiko. Hata hivyo, kwa sababu ya uwezo wao wa kurekebisha, wameweza kuyaenea kufunika milima, vinamasi vya pwani, na miji. Wakazi huwafikiria kama wanyama waharibifu. Matokeo ya utorokaji mbalimbali na maingiza ya makusudi katikati ya karne ishirini, rakuni wanaishi katika Ulaya ya Kati, Milima ya Kaukasi, na Japani. Katika Ulaya, rakuni yupo orodhani pa spishi ya migeni zinazoelekea kusambaa tangu 2016.[1] Kwa hivyo, spishi haiwezi kuingizwa kama bidhaa, kuzalishwa, kusafirishwa, kuuzwa, au kuachiwa huru mahali mwengine mwa Umoja wa Ulaya.[2]
Hata kama ilieleweka kuwa rakuni huwa pweke, sasa shuhuda zinaonyesha spishi ina tabia za kijamii ambazo ni mahususi ya jinsi. Wanawake wa spishi wa familia moja wanashirikiana eneo la pamoja; Wanaume ambao si wa nasaba moja wanaishi pamoja vikundi vya rakuni nne ili kulinda eneo dhidi ya uvamizi wa wanaume wageni wakati wa kupandana. Eneo hili linaweza kufikia kati ya hekta tatu kuhusu wanawake wa mji na hekta 5,000 (kilometa 50 za mraba) kuhusu wanaume wa mbuga. Kipindi cha kuchukua mimba kinajiri majira ya kuchipua kupitia tarehe 65, baadaye kati ya rakuni mchanga mbili na tatu (Kiingereza: "Kits") wanazaliwa. Mama wanawalea hadi wanatawanyia mwishoni wa majira ya majani kupukutika. Hata kama rakuni wafungwa au kipenzi wanatarajiwa kwishi zaidi ya miaka 20, matarajio ya muda ya kwishi jangwani ni kati ya miaka 1.8 na 3.1 tu. Maeneoni kwengi, mawindo na magari yanasababisha vifo vingi sana, wasipouawa na utapiamlo.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Procyon cancrivorus, Rakuni mlakaa (Crab-eating raccoon)
- Procyon lotor, Rakuni kaskazi (Common raccoon)
- Procyon pygmaeus, Rakuni wa Kisiwa cha Cozumel (Cozumel Island raccoon)
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Rakuni mlakaa
- Rakuni wa Kisiwa cha Cozumel
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Invasive alien species - Environment - European Commission". environment.ec.europa.eu (kwa Kiingereza). 2025-12-22. Iliwekwa mnamo 2026-01-03.
- ↑ REGULATION (EU) No 1143/2014 of the European parliament and of the council of 22 October 2014 on the prevention and management of the introduction and spread of invasive alien species (kwa Kiingereza) (2014-10-22). Iliwekwa mnamo 2026-01-03
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rakuni kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |