Kwelea
Mandhari
(Elekezwa kutoka Quelea)
Kwelea | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 3:
|
Kwelea ni ndege wadogo wa jenasi Quelea katika familia Ploceidae ambao wanatokea Afrika. Wanafanana na kwera lakini hawana rangi ya manjano. Rangi zao ni kahawia na michirizi myeusi juu na nyeupe au pinki chini na wana kichwa, kidari na/au domo nyekundu au pinki. Ndege hawa hula mbegu hasa lakini wadudu pia, hususa makinda madogo. Hulifuma tago lao kwa majani ya manyasi na hulining'inizia kitawi. Matago yao hupatikana katika makundi makubwa. Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Quelea cardinalis, Kwelea Kidari-chekundu (Cardinal Quelea)
- Quelea erythrops, Kwelea Kichwa-chekundu (Red-headed Quelea)
- Quelea quelea, Kwelea Domo-jekundu (Red-billed Quelea)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kwelea kidari-chekundu
-
Kwelea kichwa-chekundu
-
Kundi la kwelea domo-jekundu