Mbanjambegu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pyrenestes)
Mbanjambegu

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Jenasi: Pyrenestes
Swainson, 1837
Ngazi za chini

Spishi 3:

Wabanjambegu (kutoka Kiing.: seedcracker) ni ndege wadogo wa jenasi Pyrenestes katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Ndege hawa ni baina ya wakubwa kabisa wa familia hii na wana domo mfupi na nene sana. Wanafanana na madomobuluu lakini domo lao ni jeusi. Kichwa, kidari na mkia ni nyekundu na tumbo na mabawa ni nyeusi, kahawia au zaituni kijani. Hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi au matete lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-4.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu "Mbanjambegu" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili seedcracker kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni mbanjambegu.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.