Pioneer Jazz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pioneer Jazz iilikuwa bendi ya Mali kutokea miaka ya 1960.

Bendi hiyo iliibuka kutoka mji wa Bamako baada ya Modibo Keita, kiongozi wa Mali, kuanza kutoa ruzuku kwa vikundi vya muziki mradi tu watumie nyimbo za asili za kusifu, na ala za muziki za kora na balafon, katika muziki wao. Pioneer Jazz ilipata umaarufu mkubwa, na ikachangia wanamuziki waliojiunga na bendi nyingine mashuhuri za Mali.

Mwanachama mashuhuri zaidi wa Pioneer Jazz alikuwa mpiga gitaa Djelimady Tounkara, ambaye baadaye alijiunga na Bendi ya Reli.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]