Nenda kwa yaliyomo

Pio Laghi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pio Laghi (21 Mei 192210 Januari 2009) alikuwa kardinali wa Italia katika Kanisa Katoliki. Huduma yake ilijikita zaidi katika utumishi wa kidiplomasia wa Vatikani na Kuria ya Roma. Alihudumu kama Balozi wa Kitume katika nchi kadhaa na pia kama Mkuu wa Idara ya Elimu Katoliki. Aliteuliwa kuwa kardinali mwaka 1991. Kardinali Laghi alikuwa mjumbe wa siri wa Papa Yohane Paulo II katika Ikulu ya Marekani na kwa marais kadhaa wa nchi hiyo. Alikuwa na uhusiano wa karibu hasa na George H. Bush na George W. Bush.

Kazi yake kama balozi wa kitume nchini Argentina (19741980), wakati wa miaka ya udikteta, imekuwa na inazidi kuwa mada ya mjadala na utata.[1][2][3][4]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.