Pieter Brueghel Mzee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Misemo na nahau za lugha ya Kiholanzi
Mnara wa Babeli
Pieter Breughel alivyojichora mwenyewe

Pieter Brueghel (* kati ya 1525 na 1530 mjini Breda; † 5 Septemba 1569, Brussels) alikuwa mchoraji Mholanzi wa karne ya 16. Anaitwa "Brueghel Mzee" ili kumtofautisha na mwanawe Pieter Brueghel Kijana aliyekuwa mchoraji mashuhuri pia. Anahesabiwa kati ya wachoraji muhimu zaidi wa Zama za Mwangaza ya Ulaya.

Brueghel alijifunza sanaa ya uchoraji mjini Antwerpen hadi kufikia kiwango cha fundi mwalimu. Mnamo 1552-1555 alisafiri Italia alikoangalia sanaa ya karne nyingi.

Picha za Brueghel zinaonyesha vinaganaga vingi, alipenda kuficha ujumbe wake katika vipengele vidogo. Alipenda kuonyesha maisha ya wakulima vijijini kwa umakini kabisa. Picha zake zote zinasimulia hadithi katika mazingira ya mandhari ya kiholanzi. Alichora pia habari za Biblia na ndoto akifanana na Hieronymus Bosch.

Kati ya picha zake mashuhuri sana ni "Misemo na nahau za lugha ya Kiholanzi" alimoonyesha misemo zaidi ya 100, halafu pia "Mnara wa Babeli".

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: