Phyllis Omido
Mandhari
Phyllis Omido (alizaliwa Phyllis Indiatsi Omido 1978 hivi) ni mwanaharakati wa mazingira wa Kenya. Alikuwa mmoja wa watu 6 waliopewa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mnamo 2015. Alijulikana kwa kuandaa maandamano dhidi ya kiwanda cha kuyeyusha madini ya risasi kilichoko katikati ya mtaa wa Owino Uhuru, uliopo karibu na Mombasa. Kiwanda hicho kilisababisha sumu ya risasi kwa kuongeza kiwango cha madini ya risasi katika mazingira, kuua wakaazi, haswa watoto, na kuwadhuru wengine, akiwemo mtoto wake mwenyewe. Kiwanda hatimaye kilifungwa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Phyllis Omido kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |