Phillippa Yaa de Villiers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Phillippa Yaa de Villiers (alizaliwa 17 Februari 1966 [1]) ni mwandishi na msanii wa maonyesho wa Afrika Kusini, anayefanya kazi yake kitaifa na kimataifa.

Anatambulika vema kwa kazi yake ya uandishi wa mashairi iliyochapishwa kwa mikusanyiko na katika majarida mengi na hadithi. Vile vile anatambulika kwa tawasifu yake ya Original Skin iliyoeleza hali ya kutoelewa utambulisho wake akiwa mdogo kutokana na kulelewa na mama mwenye asili ya Australia na baba mwenye asili ya Ghana katika kipindi cha ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.[2] Aliandika: "nimekuwa Phillipa Yaa pale nilipompata baba yangu mzazi, aliyeniambia ya kuwa alikuwepo kipindi nilipozaliwa, na jina la kwanza kupewa lilikuwa Yaa, Yawo au Yaya lenye asili la Akan wanayopewa Watoto wote wa Ghana wanapozaliwa siku ya alhamisi. Hivyo lengo la kubadili jina langu ni kujivunia katika asili yangu ya uafrika. Baada ya kukua kama mtu mweusi katika watu weupe wa Afrika Kusini, ilisababisha kuwepo ukweli hasi kuhusiana na namna watu Weusi walivyo. Nilihitaji kuukomboa utu wangu kutoka kwangu mwenyewe kutokana na pingamizi zilizokuwepo. " [3] Alisema pia: " kwasababu sikuambiwa ya kuwa nililiewa na walezi mpaka nilipofikisha miaka 20, nilikosa misamiati ya kujielezea mimi ni nani na nimetokea wapi hivyo maonyesho na uandishi zikawa njia ya kujitambua kwangu".[4] Kama Tishani Doshi alivyotazama tovuti ya New Indian Express: "Kazi yake inahusiana sana na ujinsia, asili, na matabaka ndani ya Afrika Kusini"[5]

Malezi[hariri | hariri chanzo]

De Villiers alizaliwa Hillbrow Johannesburg nchini Afrika ya Kusini [6] Ambapo alitumia miezi kadhaa ya mwanzo wa maisha yake katika nyumba ya kulelea watoto iitwayo “the Princess Alice home”. Akiwa nusu Muaustralia na nusu mghana,[5] alilelewa na walezi weupe bila ya kuambiwa kuwa ni mtoto wa kulelewa mpaka alipofikisha miaka 20.[7] Aliandika kuhusiana na athari na uzoefu alioupitia: "Nilianza uandishi wa mashairi nikiwa mtoto, shairi langu la kwanza ilichapishwa nilipokuwa na umri wa miaka 11. Nlikuzwa kwenye familia inayopenda mashairi hususani katika lugha ya kiingereza. Nilipokuwa mkubwa ndipo nilipotambua ya kuwa uandishi ni zaidi ya maneno yanayoonekana katika kurasa. Uandishi humjumuisha mwandishi, historia yake, mambo yanayomhusu na muktadha katika jamii. Historia yangu ilichangia sana katika ubunifu wangu pale nilipoanza kuchunguza asili yangu kama mwanamke mweusi aliyelelewa na familia ya watu weupe kipindi cha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Nilihisi kama watawala na watawaliwa wanapigana ndani ya ubungo wangu."[8] [9]

Elimu ya juu na kazi[hariri | hariri chanzo]

Alisoma shahada ya uandishi wa Habari katika chuo kikuu cha Rhodes[10][11] Na pia alipata shahada ya heshima ya uigizaji na uandishi wa hati kutoka chuo kikuu cha Witwatersrand.[10] Ni mhitimu wa shule ya kimataifa ya maonyesho la L'École Internationale de Théâtre Jacques Lecoq iliyopo Paris nchini Ufaransa ambapo alisomea maonyeso.[12][13] Aliishi Los Angeles kwa mda [1] kabla ya kurudi Afrika Kusini mwaka 1998 na kuishi Johannesburg.[6] Alifanya kazi kama mwigizaji kwa miaka miwili, akifanya maonyesho na kushinda kupitia kazi zake zifuatazo, Kwamanzi, Horn of Sorrow na Elephant of Africa. Miaka nane iliyofuata, alikuwa mwandishi wa hati za runinga[7] kwa matamasha kama vile Backstage, Tsha Tsha, Thetha Msawawa, Takalani Sesame na Soul City [13]

Fasihi zilizochaguliwa[hariri | hariri chanzo]

  • Taller Than Buildings (Cape Town: Centre for the Book, 2006,
  • with Keorapetse Kgositsile, Don Mattera and Lebo Mashile, Beyond Words: South African Poetics (an Apples & Snakes project; flipped eye publishing, 2009, )
  • The Everyday Wife; foreword by Margaret Busby
  • Editor (with Kaiyu Xiao and Isabelle Ferrin-Aguirre), No Serenity Here – an anthology of African Poetry (Beijing: New World Publishers, 2010).
  • ice cream headache in my bone (Cape Town: Modjaji Books, 2017)

Kama mchangiaji[hariri | hariri chanzo]

  • "Staying Safe", Konch Magazine, Special Issue, The Virus: Volume II, 2020.[14]
  • Marike Beyers (ed.), The Only Magic We Know: Selected Modjaji Poems 2004 to 2019, 2020.[15]
  • "Research That Is Real and Utopian: Indigenous Knowledge as a Resource to Revitalise High School Poetry" (with Louis Botha and Robert Maungedzo), Education As Change, 23 December 2020.[16]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Phillippa Yaa de Villiers biography at Lyrikline.
  2. "Profiles – 8 South African Women Writers" Archived 19 Aprili 2021 at the Wayback Machine., African Writing Online, December/January 2008.
  3. "Thoughts behind Indegenius: concept for the 29th", Pulse, 8 November 2014.
  4. MarLa Sink Druzgal, "Around the World with the Poetry of Phillippa Yaa de Villiers", Traveling Marla.
  5. 5.0 5.1 Tishani Doshi, "Poetry Beyond the Edge of Time" Archived 7 Machi 2016 at the Wayback Machine., The New Indian Express, 4 October 2014.
  6. 6.0 6.1 "About Phillippa Yaa de Villiers", The Poetry Archive.
  7. 7.0 7.1 "Poets on Adoption", 11 April 2011.
  8. https://cashp.columbian.gwu.edu/woman-science
  9. Darwin's Hunch: Science, Race and the Search for Human Origins.
  10. 10.0 10.1 "Biographical note, Jozi Book Fair 2009.". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-17. 
  11. Phillippa Yaa de Villiers page Archived 7 Agosti 2018 at the Wayback Machine. at Passa Porta, International House of Literature in Brussels.
  12. "Biography at Badilisha Poetry.". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-30. Iliwekwa mnamo 2021-04-17. 
  13. 13.0 13.1 Biography at Centre for Creative Arts (CCA) Archived 7 Agosti 2018 at the Wayback Machine., University of Kwazulu-Natal.
  14. "Staying Safe", by Yaa de Villiers Amamoo.
  15. Susanna Sacks, "'A Thousand Tentative Tendrils': Review of The Only Magic We Know: Selected Modjaji Poems 2004 to 2019", Africa In Words, 5 June 2020.
  16. Botha, Louis, Phillippa Yaa De Villiers, and Robert Maungedzo, "Research That Is Real and Utopian: Indigenous Knowledge as a Resource to Revitalise High School Poetry", Education As Change, Vol. 24 (2020).
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Phillippa Yaa de Villiers kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Phillippa Yaa de Villiers kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.