Pepenazi

Opeyemi Gbenga Kayode (anajulikana kwa jina lake la kisanii Pepenazi, amezaliwa 16 Aprili 1988) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria.[1]
Maisha ya Awali na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Gbenga alizaliwa jijini Lagos na alikulia akisikiliza muziki wa Ebenezer Obey, King Sunny Adé, The Beatles, I. K. Dairo, na Fela Kuti.[2] Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Awali na Msingi ya Kemeesther iliyopo Aguda, Surulere, Lagos. Pepenazi alipata elimu ya sekondari katika shule ya Mayflower School mjini Ikenne, Jimbo la Ogun, ambapo shauku yake ya muziki wa rap ilianza kukuwa aliposikiliza nyimbo za Wyclef Jean, the Notorious B.I.G, P. Diddy, Fat Joe na wengine.[2]
Alifuzu na shahada ya Sayansi ya Teknolojia katika Usimamizi wa Ardhi kutoka chuo kikuu cha Federal University of Technology, Akure, Jimbo la Ondo, ambako alirekodi wimbo wake wa kwanza. Wakati akiwa chuoni, Pepenazi alishinda uchaguzi wa wanafunzi na kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Kijamii wa Chama cha Wanafunzi na pia alishiriki katika albamu iitwayo Futa's Finest.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kusaa. "Listen to Afropop music by PEPENAZI at kusaa.com". Kusaa. Iliwekwa mnamo 2022-10-25.
- 1 2 3 elibawa (2016-03-19). "Junior and Pretty made me become a singer –Pepenazi | Punch Newspapers" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2016-07-04.
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pepenazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |